Kusinzia ugenini maana yake nini? {swali}

nkyandwale

Member
Feb 8, 2011
64
14
kusinzia ugenini !

1. Jamani nambieni,ukweli nipate jua
Ee malenga toboeni, hata kwa kusoma dua
Hapa bara hata pwani, dhana hii pembua
Kusinzia ugenini, maana yake ni nini ?

2. Safari kuipigania, hata ndururu kutoa
Mwanaume kupania, kwa waridi kujitoa
Waridi kukaribia, hata siri kutoboa
Kusinzia ugenini, maana yake ni nini?

3. Ua kupata mgeni ,hasa mkiki murua
Mizigo kutunzwa ndani, waridi nyama pakua
Kitanda hakitamani, ujasiri humpungua
Kusinzia ugenini , maana yake ni nini ?
4. Ujasiri hupungua, maungo kumlegea
Mbio hawezi timua, usingizi kumkolea
Hutweta kwa kupumua, waama akielea
Kusinzia ugenini, maana yake ni nini?

5. Tano naweka kifungo, jibu jema nasubiri
Sitegemei magongo, na msuto wa kiburi
Akifikia ukingo, ajiona yu saburi
Kusinzia ugenini , maana yake ni nini?

Nkyandwale.
 
KUSINZIA UGENINI MAYAKE NI KUJITOA MUANGA KWA YULE UMPENDAYE KAMA VILE ANAVYOSEMA KWEYE UBETI WA
2. Safari kuipigania, hata ndururu kutoa
Mwanaume kupania, kwa waridi kujitoa
Waridi kukaribia, hata siri kutoboa
Kusinzia ugenini, maana yake ni nini?
HAPA TUNAONA JINSI GANI HUYU JAMAA ANA JITAHIDI KILA HALI ILI KUMPATA HUYO UWARIDI
 
Back
Top Bottom