Kushangiliwa maana yake nini?

Kushangiliwa maana yake nini?

Papaa Muu

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2018
Posts
243
Reaction score
292
Tarehe 25/5/2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Dkt.John Pombe Magufuli aliudhuria kuapishwa kwa mshindi wa ugombea urais wa South Africa.Wakati wa kuingia alipotajwa tu kuwa anayeingia ni Rais wa Tanzania umati ukaamka kushangilia kwa nguvu mpaka alipoenda kuketi,nini sababu kubwa ya kushangiliwa huko.

Tukiacha urafiki undugu umoja nk uliopo baina ya Tanzania na South Africa kuna jambo jipya limetokea toka aingie madarakani Rais Magufuli.

Ni miaka mingi waafrika wamekuwa wakishuhudia aina ya viongozi ambao wameshindwa kusimamia rasilimali za nchi zao na kushindwa kukemea ubadhirifu unaofanywa na baadhi ya viongozi ambao walipata kushika madaraka na kushindwa kukemea maovu kama rushwa nk.hili limewachosha waafrika nakuanza kuombea watu wakukemea haya yakatengemaa,sasa kwa Africa wamemshuhudia si mwingine ni Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.

Waafrika wameona na wameshuhudia juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.JPM ikifanya yale kwa miaka mingi yalikuwa yanaonekana kushindikana kufanywa mpaka ikasemekana labda waafrika watawaliwe tena ndio itafanyika,waafrika waliamini rushwa ni sehemu ya maisha kuwa lazima uitoe au upokee lakini Rais wa Tanzania amekuja akaanza vita na wala rushwa na watoa rushwa kwa vitendo kabisa mpaka ikawa nimfano wa kuigwa na nchi zingine huku wakishuhudia mialiko mfano ya uingereza ambayo ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na waziri mkuu wa Tanzania walialikwa kueleza namna Tanzania ilivyofanikiwa kupambana na rushwa.

Wengi wa waafrika waliamini itakuwa ngumu kwa nchi za Afrika kusimamia rasilimali zake zikaleta maendeleo lakini Tanzania chini ya Rais Dkt JPM imeonyesha mfano kuwa inawezekana kusimamia rasilimali na kuziongezea thamani kwa kuhakikisha nchi inapunguza kuuza malighafi kama malighafi bali inajikita katika kuuza bidhaa iliyokamilika ambayo ina thamani zaidina kuiletea nchi faida kubwa,hii mfano utaona wengi waliona ni ngumu kuzikemea kampuni kubwa za nje kwa kunyonya nchi changa malighafi hivyo Rais Dkt John PM alizuia makontena zaidi ya mia yenye mchanga wa madini na madini akatambulisha sera mpya ya madini akavunja mikataba mibovu isiyo na tija kwa nchi na kuwafanya hayo makampuni kuomba maongezi ya makubaliano na kukubali kulipa kodi waliyokuwa wanakwepa pamoja na fedha ingine kwa nchi,jambo ambalo ulimwengu mzima haukuamini kama linawezekanika kwa nchi changa kushindana ubabe na makampuni haya ambayo yalionekana yasiyogusika lakini Rais Magufuli kayagusa na yanabadilika sasa nchi inaona faida ya ilichonacho.

Waafrika walizoea kuona ili kufanikiwa lazima Rais kila wakati asafiri nje mara kwa mara lakini kwa sasa wengi wameshangazwa na Rais JPM ambaye mpaka wakati huu hajatoka nje ya bara la Afrika bali ameweza kuonyesha kwa nini nchi inakuwa na balozi(wawakilishi)nje,ameweza kufuta safari za wafanyakazi za nje ya mchi zisizo na tija kwaasilimia kubwa ukiacha zakemwenyewe ambapo mpaka sasa waafrika wameona kumbe inawezekana kabisa kwa Rais kutokutoka nje ya bara la Afrika akabana matumizi makubwa yanayofanyika kwasafari hizi za nje hivyo akawa na safari chache sana ambazo ukipiga hesabu mpaka sasa inawezekana Rais wa Tanzania akawa katoka nje ya nchi yake kwenda nchi zingine za Afrika haifikii hata mara mia ukilinganisha na marais wengine wa Afrika ambao hufikisha hata safari mia nne kwenda nje ya afrika.

Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo waafrika wanayaona kwa macho yao na kuyasikia na kuthibitisha kuwa kumbe yanawezekana,kwa waafrika imekuwa ni kama Rais Magufuli anarudisha heshima ya waafrika ile yakuonekana hawawezi kujiamulia mambo yao bila kuamuliwa na nchi kubwa na kuonyesha kuwa hata waafrika wanaweza wakasimamia nchi zao vizuri naa zikaendelea.Hii imemfanya Rais Dkt John P.Magufuli kuwa ndio mfano wakuigwa kwa marais wa Afrika na waafrika wengi wangependa marais wa nchi zao wafanye haya anayoyafanya Rais Magufuli kwa nchi yake.

Nani asiyejua ukweli huu juu ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais JPM inavyofanyakazi nzuri kwa Tanzania ambapo hata wachumi ndani na nje wanaona na kukiri kuwa kama Tanzania itaendelea hivyo kwa miaka kumi basi jua baada ya muda Tanzania itakuwa iko juu kiuchumi,hili hata Waafrika wanalijua na kuliona ni zuri ndio maana wanataka liigwe,wanafahamu kuwa lazima kuna wasiopenda juhudi za hivyo ila je wapo kwa kujenga pamoja kwa kutoa mbinu B katika jambo baada yakuona mbinu A ya serikali au wapo kwa kuirudisha nchi yao nyuma kimaendeleo na kuiharibu kama vikwazo vya nje vinavyojitokeza kwa propaganda za ajabu,jibu analo atakayekuwa anakwamisha hapo,ila Waafrika wanalotaka ni kuona jambo zuri la Rais Dkt JPM liigwe na kuanza kazi kwa haraka kuondoa matatizo wanayoyapata wao nchini mwao...ndio maana kila anaposimama Rais wa Tanzania watu weengi hulipuka kwa shangwe na nderemo ukiacha vifijo visivyoisha kufikisha sauti zao kuwa anayoyafanya si madogo ni makubwa na ya maana sana ambayo yanahitajika kwa dunia ya sasa.

Ndio maana sikushangaa sana maana najua watu wa Afrika wanampima Rais wa Tanzania kwa kazi zake naye kama anavyosemaga "Sitawaangusha" na kweli wanaona "Hawaangushi" bali amezidi kufanya mazuri wayatakayo.
Hongera sana Watanzania kwa kumuunga mkono.

Hongera Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa mazuri yasiyohesabika unayoyafanya katika nchi hii nzuri ya Tanzania,unatuonyesha uzalendo wa hali ya juu,hatutakuwa nyuma yako bali tutakuwa bega kwa bega kukamilisha yote.
Acha Afrika ilipuke kwa shangwe ni heshima kubwa unaipa Afrika....Asante sana
 
Jamani mbona kila rais alishangiliwa? Hata Museveni alipoingia alishangiliwa sana tu. Mambo mengine tuwe na kiasi. We love our president yes but we can not stoop low praising for such minor issues as if it only happened for our president and not to other dignitaries
 
in bora unyamaze tu, tumesema kila mgeni aliekua ameingia siku hio alishangiliwa, nyinyi mmeonyeshwa kipande cha video ya kukaribishwa rais wetu, na sio kushangiliwa huko unavyojengea hoja!
Acha ushamba! Unadhani wote wapo mabondekuinama? Watu tumefuatilia tukio zima live.
 
Mbona kila rais au mgeni aliyeingia alishangiliwa? Kwani kuna aliyezomewa jamani? Labda mngesema ni rais pekee aliyegeuka mpiga picha hapo tutawaelewa!
 
Mbona kila rais au mgeni aliyeingia alishangiliwa? Kwani kuna aliyezomewa jamani? Labda mngesema ni rais pekee aliyegeuka mpiga picha hapo tutawaelewa!
Mtateseka sana, mtapoteza hata iliyo riziki yenu. Mungu ndo mgawa riziki na humchukia mwenye wivu kwa mafanikio ya wenzie.
 
Acha ushamba! Unadhani wote wapo mabondekuinama? Watu tumefuatilia tukio zima live.
Bado mtasema "baada ya kushangiliwa, mtukufu Rais wetu alibebwa juu kwa juu kama Pele alipofunga bao la elfu moja. Hakika rais wetu anapendwa dunia nzima"
 
Mtateseka sana, mtapoteza hata iliyo riziki yenu. Mungu ndo mgawa riziki na humchukia mwenye wivu kwa mafanikio ya wenzie.
Hatujapinga kuwa hajashangiliwa ila tunasema siye yeye tu aliyeshangiliwa
 
Hatujapinga kuwa hajashangiliwa ila tunasema siye yeye tu aliyeshangiliwa
Kwa mwenye akili anaelewa vyema kutokana na tone. Watu wanajua kwa wote wameshangiliwa wanachojadili ni upekee wa ushangiliaji.
 
Bado mtasema "baada ya kushangiliwa, mtukufu Rais wetu alibebwa juu kwa juu kama Pele alipofunga bao la elfu moja. Hakika rais wetu anapendwa dunia nzima"
Wanaoweza sema hivyo ni wale wenye akili kama yako.
 
Hiyo maana umeitengeneza mwenyewe. Tukio la kupigiwa makofi linaweza kuwa na maana nyingi sana kijana usikariri
 
Jamani mbona kila rais alishangiliwa? Hata Museveni alipoingia alishangiliwa sana tu. Mambo mengine tuwe na kiasi. We love our president yes but we can not stoop low praising for such minor issues as if it only happened for our president and not to other dignitaries
Hahahaa....... Umenikumbusha alipoingia King Mswati!
 
Nasikia sio ndani ya uwanja tu, bali hata mitaani ni fire
 
Ushauri wa MALEMA kwa Ramaphosa unafaa kuigwa hapa Tanzania na Watanzania sio ngonjera za mtoa MADA,,,, nanukuu "He said the position Ramaphosa held needed people who tell him the truth at all times. He further advised him to use young politicians in the ruling party, instead of recycling those who had been in service since former President Nelson Mandela's reign. He said "Mr president we congratulate you and we hope that you will be president of a corrupt-free government and you will not subject yourself to views of functionalism. There are people who thrive through patrionising president. They tell you all you want to hear, and as a result you are unable to make informed decisions because you surround yourself with praise singers and yes men and yes women.

I've seen young men and women from the beaches of ANC may be it is time to consider them so they can come to you with fresh ideas, with new ideas and if they don't like position they will be able to be honest with you."You need someone who's going to be honest with you. The position you occupy needs someone who's going to be honest with you because those who failed were told many time that they were right even when they were wrong "Mwisho wa kunukuu.

Ndivyo tunavyotakiwa kuwa Watanzania sio kila siku kujikomba kwasababu ya njaa!!! Tukitanguliza matumbo yetu hatufiki mbali, Rais anatakiwa kuambiwa ukweli na mtoa ukweli unatakiwa kubaki na msimamo wa ukweli wako. Rais kuna mahala huwa anakosea sana hatumwambii ukweli ndo maana anazidi kuendelea kukosea. Mfungo mwema kwa waislamu wote.
 
Kwa mwenye akili anaelewa vyema kutokana na tone. Watu wanajua kwa wote wameshangiliwa wanachojadili ni upekee wa ushangiliaji.
Hivi kushangiliwa ishakuwa ni big deal kiasi cha kupandisha nyuzi? Wa Tz sijui tunakwama wapi!
 
Binadamu ana tabia ya kujikataa, sasa Rais wako kushangiliwa unachukia? ama ni ile kosa wanalofanya wazazi wetu wengi wa Ki-Afrika kutukataa tangu tukiwa matumboni?
 
Back
Top Bottom