CCM katika jitihada zake za kuiteka Katiba wametumia mbinu ya kuwanyamazisha wanachama wao walio kwenye bunge la Katiba wametumia mbinu ya kulazimisha kura ya wazi.
Walichofanya CCM ni kuangalia mambo kwa mtazamo mfupi sana na hawakuzingatia matokeo ya baadae muda si mrefu. Wamesahau kuwa kuna mambo mawili ambayo walitakiwa kuyatilia maanani hasa kwa upande wa Zanzibar.
1. Wamesahau kuwa siku zote ushindi wao unakuwa wa mizengwe kule Zanzibar au tuseme ni ushindi kiduchu.
Sasa uwazi una maana kuwa wapiga kura kwenye chaguzi na wananchi kwa jumla watawajuwa nani na nani ndio "wasaliti" wa maoni ya Wazanzibari hivyo basi wanabidi wajitayarishe na kushindwa na kunyooshewa vidole na wakazi wenzao. Hali inakuwa mbaya zaidi kwa wale wa makundi maalum wataishi vipi mitaani?
2. CCM imezoea kuwanunua wapinzani na kwa kukabiliana na hili umoja wa UKAWA utawaagiza wanachama wake wote nao wapige kura za wazi ili kuzuia usaliti kwa kununuliwa na CCM. Kwa upande wa Zanzibar wale watu 16 walioelezwa na rais hawatoweza kununuliwa.
Nategemea kuwa hii kura ya wazi itakuwa ni chaguo la vyama vya upinzani ili kuonyesha mtizamo wao wa serikali tatu na kuwafanya watakaopiga kura ya siri kuonekana wasaliti.
Acha uwongo,HAKUNA ANAELAZIMISHWA KUPIGA KULA YA WAZI,kanuni iliyopitishwa inamruhusu kila mjumbe kuamua ama ya wazi au ya siri na sio kama unavyosema eti wamelazimishwa.Na ndo maana hata mh Mnyika kapiga ya wazi.
ha ha ha ha ha ha haaaaaah! Hapa vidumu vya tindikali vinawahusu wasaliti
Mkuu, Kanuni za bunge la Katiba hazilamishi mbunge yoyote kupiga kura ya wazi au siri.
Kilichofanyika ni wabunge kupewa uhuru wa kupiga kura ya wazi kama anapenda au ya siri vile vile kama anapenda, kwa maana nyingine, kila kundi lilipata kile lilichokuwa likitaka kuhusiana na aina ya upigaji wa kura. Hakuna mbunge au kundi la wabunge kwa sasa limelazimishwa nje ya matakwa yake katika aina ya upigaji wa kura
Andiko lako linaonyesha wewe ndiyo hujafahamu kilichokubaliwa au unafahamu lakini unajaribu kupotosha wana Jf.
Ni angalizo tu.
Msingi na Kigezo cha demokrasia ni kufanya jambo kwa matakwa yako ambayo wakati mwingine unaweza kuyaweka kisheria ili kuwepo na kumbukumbu katika utendaji wake.Mfumo wowote wa KIdemokrasia unataka mtu apige kura ya siri,hii ni kutokana na kutokuwa infuenced na mtu au kitu chochote wakati wa kupiga kura.Kilichofanyika kwa CCM ni kuwanyima uhuru wana CCM wa kuvote against, kwani ilikua inaangalia ni kina nani watakao vote against.Ilikua rahisi kwa CCM wale wanaovote kwa siri ni dhahiri hawako upande wao, na wale watakaovote wazi wanajulikana.
Huu ni uhuni.Kwani viongozi wenyewe wa bunge walichaguliwa kwa kura ya siri.
Aweda umerudi lini? Karibu tena jamvini!Mkuu una hoja nzuri lakini unahitaji kutulia na kuiandika vizuri zaidi.
Bora ya mimi kuwa muongo lakini wewe kuwa mnafiki kunakusaidia nini, zile siku 40 zilikuwa za nini?Acha uwongo,HAKUNA ANAELAZIMISHWA KUPIGA KULA YA WAZI,kanuni iliyopitishwa inamruhusu kila mjumbe kuamua ama ya wazi au ya siri na sio kama unavyosema eti wamelazimishwa.Na ndo maana hata mh Mnyika kapiga ya wazi.