Ukiona unapingwa kwa kila jambo jirekebishe kuna jambo utakuwa ulikosea. Ukiwa mbaguzi usitegemee kuungwa mkono hata kwa mazuri, ukiwa mpenda sifa basi kila ufanyalo watu watasema ni kiki tu. Ukiwa kiongozi epuka mambo yanayowagawa watu, epuka uonezi na upendeleo ,usipende watu wakujue tabia zako za ndani. Watu wakisha kudharau hata uwaletee pesa watakula na dharau itaendelea tu.