Niende moja kwa katika mada,juzi kati upepo wa ajabu ajabu ulivuma na katika kipindi hicho nilikuwa na stress kama GB 10. Nikajitoa ufahamu kama mbwai na iwe huyo kwenda kupima ngoma. Nikamkuta mhudumu wa kike nikaeleza kuwa nataka kupima ngoma ,Dada akaniita chumba namba mbili yaani hakunishauri wala mahojiano huyo akaagiza nimpe kidole faster kanitoboa kaweka vitu vyake tayari kwa kupima. Nikahisi moyo unataka utokee ubavuni nikwamwambia nina haraka sana kama vipi nitayajia au anitumie. Dash!! Nadhani aligundua akanambie we tulia tu ni dk chache majibu yatakuwa tayari. Nikasema leo nimeingia cha kike na nimechuchumaa tayari. Mara akaitwa nje kakipimo kakaacha mezani mi nimekodoa macho kuhesabu mistari katika kipimo ile anakuja ndo mambo yameiva,mara huna ngoma kwa huyo kuwa makini. Kwa kweli kutoka moyoni nilijihisi nimekuwa mwepesiiii kama mtoto mchanga.
Wadau kupima ngoma ni mtihani ambao hata Dr.anaweza kufeli. Jamani tutulie na wenza wetu