pia
menya mihogo yako
kata vipande vidogo vidogo huku ukiutoa ule mzizi wa katikati
ioshe vizuri kisha iweke katika sufuria unayotaka kupikia
kuna nazi chuja tui bubu pembeni lile tui la pili lichujie kwenye mihogo
hapa hakikisha tui lipo level moja na mihogo sio tui pwaa katia kitunguu maji kiasi kisha bandika jikoni
maji yakianza kukauka mimia tui lako bubu acha lichemke kiasi liive kisha tegua,
badala ya kuweka kitunguu waweza miminia duvi humo sio lazma samaki wa kukaanga hata wa kuchemsha na mbirimbi, embe au limao na chumvi vikaukie mtegua utakula had uvimbiwe