TL. Marandu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 3,625
- 5,810
Huko siku za Nyuma, Nilishawahi Kulalamika sana Kuhusu wabunge wa Upinzani, Kukamatwa Hovyo na Kupigwa wakiwa katika shughuli zao huko Mitaani. Hiyo ilikuwa ni Katika Serikali za Kikwete. Ungelitegemea Magufuli niliyemdhania kuwa Muugwana, Mkweli, Mpenda haki, angekomesha tabia hii chafu.
Lakini sasa wahuni kama Chenge wanaleta FFU bungeni Kupiga Wabunge ati kwa Kuwa wamekataa kutoka nje. Solution ya Kitu kama hicho ilikuwa rahisi sana, kuahirisha kikao na kufanya majadiliano ya kuleta ufumbuzi wa swala lililoleta mgongano. Sasa kwa Kuwa FFU ni Jeshi la serikali, na Rais amekaa kimya, inaonekana aliagiza hilo au hata kama hakuagiza lilimpendeza. Mimi naona Linamchafua sana Ndani na Nje, Ni aibu kwa Utawala wake ni Dharau kwa wananchi.
Haya yamewezekana kwa sababu ya Utawala wa "milele" wa CCM Unaoamini kutawala kwa Nguvu za DOLA na Wizi wa Kura na Mizengwe. Tabia hii Italifikisha Taifa Pabaya na siku Moja CCM watakosa muda wa Kujutia.