MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Kwa mwenye akili timamu akimsikiliza Mh Zitto Kabwe wakati akichangia bungeni ataelewa ni wapi aliko Ben Saanane, haina haja ya kumung'unya maneno, tuukatae uonevu huu.Ben Saanane kwa mujibu wa hotuba ya Zitto sio wa kutafutia porini wala kwenye mito au madimbwi ya maji bali maelezo na hoja zake zimeshatoa jibu.
Katika hotuba yake Mh Zitto alisema kua kila zinapofuatiliwa suala hili polisi, majibu yanayopatikana ni kwamba taarifa za simu yake zinsonesha kua siku ya kupotea kwake alikua Tababta, baadae Mikicheni ambako inasemekana ilikaa muda murefu na mwisho kabisa ikawa Mburahati na kupotea moja kwa moja,Zitto alizidi kusema kua "ukifuatilia zaidi polisi haupati taarifa za kueleweka ispokua nao wanasema kua inaonekana Ben Saanane ni kama amechukuliwa na usalama wa taifa".Ama kwa hakika jibu juu ya huyo ndugu yetu liko wazi.
Pili ukisikiliza maneno ya ndugu Nape Nnauye ambaye juzi tu alikua Afisa ngazi ya juu serikalini, bado unaweza kuunganisha dots ukapata jibu.Nape kama alikua ni kiongozi wa srikali ni imani yangu kua anafahamu mengi sana juu baadhi ya mambo yanayiendelea serikalini wala asingebwatuka bure kule jimboni kwake Mtama ambapo alilalama sana kupotea kwa Ben Saanane.
Wadau,watu wa haki za binadamu ni wa kati wa kupaza sauti kwa kuzifanyia kazi taarifa za Zitto Kabwe ili huyu Binadamu Ben Saanane apatikane.Haina haja ya UTG kupiga kele sana ilihali pa kuanzia pako wazi.