gabriel sanya
Member
- Jan 15, 2014
- 6
- 1
. Na pia kama ni askari kwa jeshi la Tanzania lenye 4 star general muundo wake unajulikana na hata idadi ya askari inajulikana pia. Mtoa mada embu funguka zaidi
Bila shaka yule aliyekuwa kwa Bwana Mkubwa hajafurahia hicho cheo kwa mwaka huu, pengine ingelikuwa mwaka kesho baada ya kuwa wameshazunguka duniani kuaga. Mafao ya kuzunguka ughaibuni sidhani yanalingana na yale ya kuketi pale Ngome. Pengine angeulizwa kabla, angeshauri abaki hapo hapo na cheo kile kile cha awali hadi Oktoba 2015! ni mtazamo tu!
Hilo hata sisi huku Israel tumeliona kuna dosari kubwa sana katika upandishaji vyeo aina hii, hata hivyo Mods weka hii katika jamii Intergence tufunguke kwa uwazi zaidi athari zake.
Takribani miaka minne iliyo pita upandishwaji vyeo vya maafisa wakuu ( Brig Gen )umekuwa ukifanyika bila kufuata !!MUUNDO WA JWTZ'' Muundo kwa maana ya ukubwa wa jeshi idadi ya nguvu kazi iliyopo, ikijumuisha askari na silaha.
Tafsiri iliyopo inaonekana vyeo vinatolewa kama zawadi na sio kwa kufuata Merits. Inashangaza kuona jeshi linakuwa na majenerali wengi ambao hawafiti kwenye muundo., athari zake ni serikali kujibebesha Mzigo wa fadhila uchwara. Baadhi au wengi wao wanaishi kwenye nyumbani za kupanga uswahilini ambazo pengine hazina hadhi ya chao chake na huenda pia hazipo katika maeneo yenye usalama. Kwa maana nyingine watahitaji nyumba zilizo kwenye maeneo salama.
Kwa ukubwa na idadi hiyo watahitaji magari aina ya mashangingi yeye nyota za shaba kwa ajili ya utambulisho. Mishahara minono, ofisi, samani za ndani kwa entitlement zao. Sura ya kupandisha vyeo kama zawadi au fadhila inakuja kuonekana pale afisa mkuu huyo anatumika kwa muda wa mwaka mmoja tangu apate cheo anafikia kikomo cha mda wake wa kustaafu utumishi jeshini. Baadhi ya magazeti yameandika wakistaafu watalipwa billion 3 kwa mkupuo.
Kama mfumo ni huo je askari wetu na maafisa wadogo tutawapa fadhila gani wakikaribia kustaafu?
Na hawa ndio watendaji halisi.
Tutafakri !!!!
Nashukuru kwa hizi taarifa japo binafsi sijaelewa nini maana ya kuzileta hapa. Kupindishwa vyeo karibu na kustaafu ni jambo la kawaida sana kwa kipindi hiki. utakuwa hutendi haki ukiwa angalia JWTZ peke yao. Labda katiba mpya yaweza kupunguza adha hii kwa kiasi fulani.
Mkuu gabriel sanya heshima sana,
Rais Kikwete ni amiri jeshi mkuu kwa mujibu wa katibu ya JMT anayo mamlaka kamili ya kupandisha cheo wanajeshi.Mpaka hapo sioni kosa alililofanya.
Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali Tanzania inakisiwa kuwa na idadi ya wanajeshi (active personnel) 27,000 - 30,000 tu.Tanzania pia inakisiwa kuwa na jeshi la akiba (reserve personnel) 80,000 - 100,000 tu hawa ni wale waliopitia jeshi la mgambo,JKT na askari wastaafu wenye nguvu.
Ukubwa wa jeshi ni kigezo muhimu sana unapotaka kupandisha vyeo askari.Kigezo kingine ni uwezo wa kiuchumi pia uangaliwa sana.Kama uchumi wako si mzuri sana kuweza kuhimili matumizi yasiyoweza kuepukwa kama mishahara inayokidhi mahitaji muhimu,vifaa vya kisasa na nk.Kigezo kingine ni hali ya usalama,ikiwa nchi iko katika hali yakuweza kuvamiwa ni lazima bajeti iongezeke mara dufu hapa nazungumzia vifaa na kuongeza idadi ya wanajeshi.
Ukiangalia idadi ya wanajeshi wetu na idadi ya mageneral haziendani hata kidogo, unapokuwa na Lt General 4. kama kumbukumbu zangu ziko sana kuna mkuu wa utawala jeshini Lt Gen S Ndomba, kuna Lt Gen mwingine yuko ofisi ya waziri mkuu (maafa) kuna Lt Gen Mwingine ni mkuu wa chuo cha taifa cha ulinzi kuna mwingine sikumbuki akapachikwa wapi.Ukienda kwa Major General labda sasa wanaweza kufikia 20 ukishuka ngazi ya Brig General wanaweza kufikia 50 au zaidi.Mfano chief of personnel ni Major General na director wake ni Major General.Ukijakutazama idadi ya Brig General utakuta wengi hawana kazi zinazoendeana na majukumu yao sana sana utakumbana na siasa mtindo mmoja