Kupanda kwa bei ya umeme

ndusi

Member
Jul 12, 2016
30
18
Wapendwa wenzangu wa JamiiForums, bila shaka tumekuwa tukisikia habari za Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kutaka kupandisha gharama za umeme.

Wapendwa nadhani hii si sahihi hata kidogo kwani tuliambiwa faida za kuanza kutumia gesi yetu ni;

1.Kuwa na umeme wa uhakika.

2.Kuwa na umeme wa bei ndogo.

Ni kweli kwa sasa tuna umeme wa uhakika lakini kupandisha bei kwa kigezo cha wao TANESCO kuuziwa gesi inayopatikana nchini mwetu kwa dola na mwekezaji si uungwana hata kidogo.

Wanatakiwa kuangalia mikataba yao na siyo kutaka mwananchi ndiye abebe mzigo huo. Jambo lingine wafanyakazi wa TANESCO nchini kote kila mtu anapewa umeme unit 700 kwa bei ya sh 5000 tu.

Sidhani kama kuna marekebisho yoyote yaliyofanyika kwa hili, kwa hiyo kama litaangaliwa vizuri hili aidha wafanyakazi kulipia umeme wanaopewa au kupunguziwa hizi Unit wanapewa angalau hata kutoka 700 hadi 200 au 100 hivi hakuta kuwa na haja ya kuwapandishia watu umeme.

Nawasilisha.
 
Hili la watumishi wa TANESCO kutumia umeme bure ni jipu linalotakiwa kutumbuliwa. Hivi kweli watumishi wa umma wote kwenye taasisi / idara wanazofanyia kazi wangekuwa wanapata bure huduma wanazozitoa/ kuziuza ingekuwaje? Yaani kwa mfano wa idara ya afya watibiwe bure, wajenzi wa TBA wajengewe nyumba zao bure, walimu watoto wao wasome bure, wa maji wapatiwe maji bure, watengeneza sukari wapatiwe sukari bure, wa BOT wapatiwe fedha bure kwa unit 700 za fedha/ month na kadhalika?

Hili la watumishi wa TANESCO kutumia umeme bure ndilo linalosababisha kila wakati watake kupandisha bei ya umeme kila kukicha kwani wao hawajui machungu yake. Hawajui kuwa kwa sasa familia ya kawaida inayotumia umeme kwa kupikia, taa, fridge 2, washing & drying machine, TV 2, computer 2, water heaters na aircondtitioners inalipa shs 900,000/ hadi 1.2 m kama bili ya umeme kwa mwezi sawa na mshahara mzima wa graduate wa digrii kama si kuzidi.

Sasa TANESCO wanataka watu wasiwe na hivyo vitu majumbani mwao? Mbona ni vitu vya kawaida tu kama tunataka maisha bora kwa kila mwananchi. Na vitu hivi vimejaa madukani kwa bei nafuu kabisa lakini ukivinunua unashindwa kuvitumia kwa sababu ya TANESCO. Ndiyo maana watu na heshima zao walikuwa wanachezea mita za TANESCO. Wamefunga LUKU bado wanapandisha bei. Kinachotakiwa ni kuteremsha bei hizi kwa kiwango angalao cha 50%.

TANESCO ni kikwazo kikubwa cha maisha bora ya wananchi. Ni muhimu nao walipe bili za umeme kwa kiwango hicho hicho kama sisi kuanzia Mkurugenzi wao. This will bring senses into their minds.

Halafu tunataka watu wasikate miti kulinda mazingira. Wataachaje kukata miti ili wapate nishati angalao ya kupikia chakula? Umeme tumeusambaza hadi vijijini kwani ni wa nini? Kwani ni wa kuwashia taa tu? Mbona kuna taa nzuri tu za mchina za bei nafuu zinazotumia mionzi ya jua. Si kwamba tunapeleka umeme hadi vijijini ili kuboresha maisha ya hawa wananchi wakawaida? Ili angalao nao wawe na ka TV angalao ka inchi 12 badala ya redio ya mbao, wawe na angalao na kajiko ka plate moja badala na kuhangaika siku nzima kutafuta kuni na kuwa na macho mekundu kwa kupuliza mafiga? Sasa hili litawezekanaje kama kutumia vitu hivyo itabidi walipe TANESCO some Tshs 100,000/ au zaidi.

Hili jambo serikali ya awamu ya tano inawabidi walivyalie njuga kweli kweli.Bei zitelemke by at least 50%. Mikataba mibovubovu ya umeme kama ya IPTL, Dowans, Songas etc ifutiliwe mbali hata kama tutalazimika kuwalipa. Plants zote za kuzalisha umeme zimilikiwe na serikali. Hayo makampuni yaliyokuja kutuuzia umeme wa dharura yaondoke kwani dharura ilishakwisha kitambo. Ulishaona wapi dharura inakuwa ni ya kudumu kama si pale TANESCO tu? Waondoke tutawalipa pole pole tukitaka. Tusiogope kupelekwa mahakama ya kimataifa ya biashara: watatuelewa tu kwani tumenyonywa sana na haya makampuni.
 
Ni shirika pekee Tanzania ambalo wateja ulipia gharama za kupata huduma. Kwa kuuziwa vifaa na mpaka mwisho wa mkataba mwenye mali anabaki Kuwa huyo huyo alieuza.unauziwa nguzo, nyanya,mita alafu bado kila kitu ni Mali Yao, anyway maswli kuhusu Tanesco ni mengi mpaka unaweza kupata wazimu
 
Da! nimeipenda hii ya kuuziwa nguzo mita halafu mwisho wa siku vitu hivyo ulivyouziwa ni mali yao!!!
 
Tanesco wameshindwa KAzi..ile nilikua danganya Toto kumbe UCHAGUZI UMEISHA SASA WATUWAFANYE KAZI mmh ndio TzYetuu
 
Tanesco ni moja ya sababu za maisha duni ya mtanzania
Jamani hapa mkumbuke kuna deni ambalo standard chatared Bank ya Hong Kong ilishinda kwenye kesi ya msingi ambayo pesa zake zilikuwa zinahifadhiwa kwenye escrow account pale BOT pesa hizo ziligawanywa kabla ya maamuzi ya mahakama!ambapo pesa hizo kama bado zingekuwepo kwenye escrow account zingelipwa kwa standard chatared Bank waliokuwa wanaidai TANESCO kupitia IPTL,pesa zimeshaliwa na wajanja na mahakama imeamuru TANESCO walipe, sasa hawa TANESCO wanataka kutuangushia jumba bovu huu ni uonevu wa mchana kweupe kwa wa TZ
 
tanzania tuna misitu mingi sana inayo faa kwa nguzo za umeme lakini mpaka saizi mwanachi anauziwa nguzo hata watu wa nje wana tushangaa sana
 
Back
Top Bottom