jaba jumah
Senior Member
- Sep 24, 2015
- 150
- 50
Pamoja na mafanikio ya kukua kwa uchumi na ongezeko la huduma za kijamii yaliyopatikana katika kipindi hiki, bado ipo changamoto kubwa ya umasikini wa kipato na usio wa kipato. Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 28.2 ya Watanzania ni masikini.
Wengi wa wananchi ha​o wanaishi vijijini (asilimia 75) na wanategemea kilimo katika maisha yao. Wapo pia wananchi masikini wanaoishi mijini ambao wanaendesha maisha yao kupitia shughuli za biashara ndogo ndogo zisizo rasmi.
Katika kupambana na changamoto hii, CCM itazielekeza Serikali zake kuboresha maisha ya wananchi wote na hususan wa vijijini, kwa kuchukua hatua zifuatazo:-
-Kuhamasisha kilimo kupitia kauli mbiu ya Kilimo Kwanza kwa kuwawezesha wakulima kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa, pembejeo, zana za kisasa na wataalamu wa ugani pamoja na mbinu za kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao;
-Kuongeza kasi ya kupima ardhi yao na kuwapatia hati miliki za kimila ambazo watazitumia kama dhamana ya kuwawezesha kupata mikopo ya kuendeleza shughuli zao za kilimo, ufugaji na uvuvi;
-Kuendeleza juhudi za kuimarisha huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, umeme na ujenzi wa nyumba bora; na -Kuongeza kasi ya kurasimisha biashara na kuwapatia wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufanyia biashara, leseni na fursa za kupata mikopo yenye masharti nafuu.