Kuongezeka kwa bei ya bidhaa zinazouzwa katika masoko ya vyakula...

Mar 5, 2016
9
4
Wafanyabiashara toka Kenya ndio chanzo. Wafanyabiashara toka Kenya wamekuwa wakijipenyeza kwa siri hadi mashambani kwa wakulima na kununua mazao Kama mahindi vitunguu na vyakula vingine kwa bei za juu ambazo huwafanya wafanyabiashara Wa ndani kushindwa kipata bidhaa kwa bei ya kawaida.

Hivyo kupelekea na wao kuuziwa bidhaa hizohizo kwa bei wanazonunulia wakenya...matokeo yake walaji wa kitanzania huuziwa bidhaa kwa bei ya juu zaidi ya ile iliyotarajiwa.

Taaarifa zisizo rasmi toka masoko ya mjini Dodoma zinasema kuwa wakenya hao huingia kwa kificho hadi mashambani kwa wakulima Wa kitanzania na kununua mzigo kisha kuyoweka nao nyakati za usiku huku wakikwepa kulipa kodi na ushuru husika Kama wafanyabiashara Wa nje.

Inasemekana wakenya hao wengi huja Mkoani Dodoma na Manyara..na kufanya uharamia huo Wa biashara.

Binafsi nadhani mamlaka husika zishirikiane na uhamiaji kufuatilia ukweli Wa jambo hili.
 
Back
Top Bottom