Kuongea na simu na mtu usiyempenda yataka moyo!

nimevuta picha hiyo lafudhi ya kimakonde nimecheka sana haha eti leta swaga mwana .Kuna ndugu yangu huyo hanaga story yeye kazi yake kusema enhe!mambo mengine?unajibu ni poa anakwambia leta storyunamjib ah hakuna story anakwambia tena, mambo mengine vipi lakini?
Imebidi nimsevu MAMBO MENGINE
 
Kuna jamaa alishanipigia usiku mkubwa sana hadi nikahisi kunaweza kuwa na tatizo kubwa that's why kapiga midnight.

Sasa wakati napokea simu..jamaa ananiambia "leta swagga mwana" kwa lafudhi ya kimakonde...Daah! Nikawaza huyu jamaa kanipigia this late night then anasema leta swaga tena? Nikamvumilia then nikamuuliza unasemaje? Akasema cheka yake ilitakq kuisha hivyo akaamua anipigie ili aimalizie!?

Nilikuwa namheshimu but nikavurumusha tusi then nikazima simu nikachapa mate hadi asubuhi.

Kuna watu wanakera sana.
Sana yani unaweza kusema wanakaribia kuwa vichaaa hawana akili ya kujiongezaaa
 
Nimekutana nayo kwa mfipa mmoja hivi kuna makabila yana tabu jamani jitu unaliambia Mimi tayari occupied lakini bado tu limekomaa daah hapo akipiga napokea sim naiacha chumbani mwenyew natoka zangu nje spendagi ujinga mim
Wafipa kama waha tu atakupa story la ziwa Tanganyika.mpaka ukome
 
Ndo Yale mtu ndio anakutongoza hata kukubaliwa bado ataanza jisemesha oohh nikutumie nauli uje Mara unakula kiasi gani kwa mwezi anajisemesha vitu wala havimuhusu
Mwingine atakwambia nimeshakuweka kwenye bajeti yangu ya mshahara kuanzia mwezi huu dadeki sipendi kauli ya "unakula sh ngapi kwa mwezi"
Utazani amewahi kukuona unalia njaa
 
KAMA KAFALLINLOVE MWENZAKO JE?? ALAF UNACHEZEA BAHATI, WENZAKO WANAZITAFUTA, MKUBALIE MWENZAKO JAMANI TUJE TULE ANGALAU WALI SIKU YA HARUSI, AKIJA KUJINYONGA KWA SABABU KAKATALIWA USIJE BAADAE UKAJILAUMU
sitaki kabisaaa kusikia
 
Back
Top Bottom