Kununua karatasi nje ya nchi ni uzembe wa kujitakia

STEVEN SIMEON

Member
Apr 7, 2016
62
35
Sioni ni kwa sababu gani Tanzania iendelee kuingiza karatasi kutoka nchi za nje kama Afrika Kusini wakati tuna kiwanda kikubwa ambacho kama kingeweza kuzalisha kwa kiasi kikubwa na kutosheleza soko la ndani na la nje, Tanzania ina miti mingi ambayo inaweza kutumika kuzalisha karatasi , sasa hao waliopewa kiwanda hicho , hao wadhindi kama wameshindwa kutosheleza soko la ndani na kuuza nje wanyang'anywe na wapewe watu wengine wenye uchungu na Taifa hili ,hao waliopo wameshindwa kazi na wanalitia Taifa hili hasara kubwa .

Kwani ni aibu kwa Tanzania kuingiza kiasi kikubwa cha karatasi kutoka nje wakati nchi ina raslimali miti ya kutosha inayoweza kuzalisha kiasi kikubwa cha karatasi kwa soko la ndani na kuuza nje , hivyo wio kwa waziri wa viwanda na Biashara kutumbua majipu ili kiwanda kiweze kujiendesha kwa ufanisi.
 
upo sahihi Tanzania ina miti mingi kuriko South Africa hilo ni deal la baadhi ya watu maana huyo anaetoa karatasi kule kaweka hela ya kutosha katika kile kiwanda Mtanzania yeyote hawakubali kumuuzia wakijua analeta Tanzania...Rotatrim paper.
 
Nchi yetu tunaipenda ila mambo yake siyo! Karatasi achananayo zungumzia njiti za meno za kuchonga tu kutoka china!!!

Unaweza kusema kwanini tusimodify miiba ya kuporini kuliko kuimport vitu kama Njiti?
 
Nakifahamu kiwanda cha karatasi mgololo.Nilipata bahati miaka ya 80 kutembelea kiwanda chote .nilijionea mwenyewe production ya karatasi mechanical ,and chemical .nilipatwa na hofu pale kiwanda kilipoanza kusua sua miaka ya tisini kwani uzalishaji niliouona pale ulikuwa mkubwa sana.Nilielezwa jinsi karatasi zetu zilivyokuwa na soko barani afrika.kiwanda cha karatasi mgololo kilikuwa kiwanda cha pili kwa ukubwa na production,cha kwanza kilikuwa kiko misri
inasikitisha sana tena sana kuuwawa kwa kiwanda hiki wauwaji wa kiwanda hiki ni kama wauwaji wa tembo,na rasilimali nyingine za nchi yetu
 
Back
Top Bottom