Mgombea Urais wa Chama cha Wakulima (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru, amesema baada ya takribani siku 40 za kampeni, anadhani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, kuna uwezekano wa kushinda kwa asilimia 75.
Kauli hii aliitoa mkoani Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari.