Kitu ambacho wengi tusichokiona ni nini vyanzo vya majanga bali tunapenda kudandia matukio yafuatayo!
Ukitazama kwa undani mathalani filamu hiyo ya kifedhuli kwanini imetangazwa tarehe inayohusiana na siku ya kulipuliwa WTC? Je nini kimejificha nyuma ya hilo? na kwanini litengenezwe na kuanzishiwa tarehe hiyohiyo? kama itatuwia vigumu kupata majawabu hapo haya basi na tujiulize ni kitu gani kilifanya kiwanda cha madawa cha Sudani kilipuliwe kwa mabomu!? Je nini kinawafanya hao waheshimiwa wanaoogopwa sana duniani waendelee kufanya mauaji kwa kutumia drone Afghanistan, Yemen, Pakistan na Somalia na kwanini si Turkey, Greece na Spain ambako pia kuna maandamano!?