Kunani bandari ya D'salaam

sir j

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
317
212
Wana Jf, habarini za wakati huu.....
Katika pitapita zangu hapa mjini kwetu, (sio D'salaam) nikawa kwa jamaa yangu mmoja mwenye kumiliki duka la simu. Akanambia, bwana eeh, kuna simu imeingia ni Tecno C10 lakini haiingilii kwa bandari ya dar, mzigo umeingilia Nairobi, na alikuwa yupo kwenye 'process' ya kuuchukua mzigo huo, kwani tayari alishatuma mtu kuuchukua (Nairobi).

Nikaamuuliza kwa nini usipitishie tuu bandari ya nyumbani (Dar_ Tz). Akanambia, rafiki, mzigo ukiingilia Dar utalia, kuja uuchomoe pale bandarini ni shida, halafu kupitishia mzigo pale, unachelewa sana kuingia sokoni.

Sasa nikabakiwa na maswali mengi pasi na majibu,

-kwamba kuna matatizo yapi bandarini ambayo yanasababisha wafanya biashara kuhamishia matumizi ya bandari kutoka dar mpaka Mombasa.....?

-Kwa nini mizigo icheleweshwe kupewa kibali cha kuondolewa hapo bandarini...?

-Je, hapa uongozi wa bandari (kama ndio chanzo) hawaoni kuwa wanawasababishia hasara wafanya biashara....?

-Je, serikali haioni kama inapoteza mapato mengi ya kuinua uchumi wa nchi kwa sababu za ajabu ajabu......? na je, ni hatua zipi zinachukuliwa/zitachukuliwa ili kukomesha tatizo hili na kurudisha imani kwa wateja wetu ili mizigo bandarini iongezeke na hatimaye kuinua uchumi wa taifa?

-Je, kwa nini wafanya biashara (kama ndo chanzo cha tatizo) kwa nini msifuate procedures zote muhimu ili mpate huduma kwa wakati.....?

Karibuni kwa mjadala huenda tukapata suluhu nzuri kwa changamoto kwa bandari zetu.
 
Me najuaga sim husafirishwa kwa njia ya ndege.. Sasa zikipita majini mzigo si utafika ukiwa outdated
 
Back
Top Bottom