Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,272
- 21,448
Mara nyingi watu wamefikia hatua ya kumlaumu Magufuli kwamba anatumbua sana watu mara nyingine hata kupita kiasi.
Ukweli ni kwamba kwa hali ambapo nchi yetu ilipokuwa imefikia, wengi tulitamani tumpate raisi kama Magufuli - kwa miaka kama kumi tuwe na raisi ambaye ana nia moja tu, kurekebisha Tanzania kwa udi na uvumba. Tanzania ilioza mno, hasa katika maadili ya viongozi, kuanzia ngazi ya ikulu hadi serikali ya kitongoji. Kikubwa kinachohitajika kwa sasa ni uzalendo wake katika suala la Hapa Kazi Tu!
Ni kweli kwamba kuna baadhi ya watu wataumizwa au kutumbuliwa na Magufuli bila kuwa na hatia, kwa namna moja au nyingine. Tunasikitika juu yao, lakini katika vita, mara nyingine ili nchi ikombolewe lazima kutakuwa na "casualities of war", wahanga wa vita, ambao mara nyingine ni raia wasio na hatia. Hata hivyo, ushindi wa vita ukipatikana wote tunafurahi na kushangilia!
Lakini pia kuna watu wanatumbuliwa, na ikiwa Magufuli angeeleza undani wa makosa yao, tungeshangaa sana kwamba hivi Watanzania wanaojiita viongozi wetu, wanawezaje kufanya mambo kupita kiasi kwa namna hiyo! Huenda hata tungetaka baadhi ya hao watu wafungwe jela maisha!
Kwa mfano, kuna balozi wetu katika nchi tajiri alipewa msaada kuleta Tanzania, akaamua kufikisha asilimia 28% tu ya msaada huo, na ile nyingine 72% akagawana yeye na vigogo wengine wa serikali. Sasa katika awamu nyingine hili suala wala lisingekuwa jambo kubwa, lakini Magufuli alipolipata akawatumbua kuanzia huyo balozi na wengineo waliopewa mgao, bila hata kuwaambia wananchi sababu!
Kuna wizara fulani ilikuwa ili upewe cheo katika uongozi wa wilaya unamkatia Katibu Mkuu na Msaidizi wake Tshs 10M, katika ngazi ya mkoa Tshs 20m. Yeye na msaidizi wake wametumbuliwa!
Hivyo Watanzania wenzangu, tumvumilie Magufuli, tumpe ushirikiano unaostahili. Maumivu yanaweza kuwapo kiasi, kama vile tu kufanyiwa operation ili kuondoa ugonjwa, lakini mwisho wa miaka kumi kila mmoja wetu atafurahia sana matunda ya kazi ya Magufuli, na Tanzania itakuwa nchi mfano wa kuigwa Afrika na hata duniani.
Tuvumilie ndugu zangu Watanzania. Tumuunge mkono Magufuli, anafanya haya yote kwa ajili ya Watanzania, sio kwa ajili yake binafsi.