Sikujua kama kuna wapuuzi duniani wa aina hii . kama unataka kubadili mambo lazima uwe katika duru.Nini kagoda wewe kuna makubwa zaidi. Lakini huwezi kukurupuka tu na kusema kama vile unafuata maji ya bahari ambayo uwa yanakupwa na kupwelea wakati huo huo lakini yakighaiori ujazo kwa kuelemea upande mmoja kubalansi dunia. Haki hupatikana ama kwa kura ama bunduki na siku zote bunduki haitoi haki kwa kuwa aliyeua hudhani wapow atakamkamua na kumuuliza kwanini umeua.Nyie mnaokataa kuingia katika kiulinge cha kupiga kura msiwafadhaishe wenzenu waache waamua.Nyie mnatufanya tusiwe na sauti hapa nchini.Plato alisema wanaume ndio wanaoamua mambo ya Athens na lazima wapige kura. Usikimbie kivuli chako ukabaki unahema siku ukionyeshwa mwanga kamili.Usipotumia kura unataka kugeuza somalia kwa kujaza hasira zisizokuwa na ukomo?Kura yako hata kama haitatosha itawapa watu salamu za heri au shari.Nenda kapige kura iwe Kagoda au kijigoda bila kuingiza wa kutosha bungeni utaendelea kuwa chizi mpaka kiama
Tanuru,
Kaka jitahidi twende si busara kususia uchaguzi - maana ukisusa wenzako wanakula - hawatakuonea huruma hata kidogo, please change your mind and move on.... Kumfikisha kagoda mahakani ni sawa na kuifikisha serikali yetu kwa pilato - jambo hili halitawezekana kabisa. kumbuka Bunge limeshindwa kumjua Kagoda ni nani? Chief haya ya kagoda, Richmond, Mwananchi gold, Melemeta, Tangold, Buzwagi, TRL na mengineyo yasituvunje moyo - Lets go guys...
Ambao hamjajiandikisha kupata kipande cha kupigia kura kama mimi please do that before saturday 27th.
sisi wenzio tutapiga, tena tutapigia upinzani wala si sisiemu. wewe mwenye msimamo wa kukubali kushindwa vitani, endelea na msimamo wako, ila jua watu wa aina yako wanaweza kuwa ni wachache sana, kiasi kwamba hawana effect yoyote kwenye taifa letu. bye.
Hivi Watanzania wote wakishawishika kutokupiga kura, kutakuwa na uchaguzi?
Silaha ya mlalahoi ni kura yake. Akiamua kuitumia vema, akasema, sipigi kura mpaka hiki, na hiki, na hiki, na hiki, kifanyike, je, atakuwa amefanya sahihi ama la? Je, mlalahoi wa Tanzania ana ujasiri huo wa kususia uchaguzi?
./mwana wa haki

Kwanza umejiandikisha?Wakuu,
Kama hali ya mambo itaendelea kuwa mbaya zaidi sitegemei kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Ni ushauri tu best, binafsi sitaweza kupiga kura kwakuwa bado niko nje ya nchi na ningependa sana kupiga kura. Ni hivi, Usipopiga kura unaruhusu viongozi WABOVU tulio nao waendelee kuongoza katika ubovu na uovu wao. Best piga kura!
SIO UPUUZI
kupiga kura kuna maana kama
mpigaji kura anapata choice ya kuchagua,kama
anaona hakuna right choice,kutopiga kura pia ni aina
nyingine ya kutoa maamuzi.....
kama kuna pepsi na coca unaambiwa uchague,unaweza sema sichagui yeyote..
which is very understandable.......
Wa kumpigia kura mwenyewe ni yupi? Kama huna chaguo ni bora tu kutoshiriki kuliko kupoteza muda wako bure.