Kuna utulivu si amani

Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,540
Likes
27,589
Points
280
Age
48
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,540 27,589 280
TANZANIA hakuna amani nchini isipokuwa kuna utulivu, hivi ndivyo anavyosema Bunga Dettu, Mchungaji wa Kanisa la Waadventista (Wasabato) Mtaa wa Dodoma, anaandika Dany Tibason.

Mbali na hilo mchungaji huyo anasema “amani ya nchi haiwezi kupatikana kwa kutumia maguvu na mabavu kwa kuwatishia wananchi.”

Katika mkutano huo amesema, kama wananchi hawataweza kupata nafasi ya kutoa dukuduku zao kwa kunyimwa uhuru, kuna uwezekano wa amani kutoweka.

“Lazima ijulikane wazi kuwa wananchi wanataka kuona wanatendewa haki katika kutoa mawazo yao na kutumia rasilimali walizonazo kwa usawa.

“Lakini kama wananchi wataendelea kuona rasilimali za nchi zinatumiwa na watu wachache huku watu wengu wakiendelea kutaabika, kamwe amani haiwezi kuwepo”amesema Mchungaji.

Abrahman Ahmed, Mwakilishi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmaddiya amesema, jumuiya hiyo ipo kwa ajili ya kukuza uhusiano mzuri kati ya jamii na serikali.

Sambamba na hilo amesema, kazi kubwa ya jumuiya hiyo ni kuhakikisha dini zote zinakuwa na uhusiano mzuri katika kudumisha amani na utulivu sambamba na kuliombea taifa na viongozi wake.
 
Odhiambo cairo

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
9,075
Likes
10,639
Points
280
Odhiambo cairo

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
9,075 10,639 280
Walitakiwa viongozi wa kiroho kuwa na misimamo ya namna hiyo. Lakini ajabu walio wengi wako dhidi ya wananchi !!!

Sitashangaa wakiitwa kuhojiwa
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
14,088
Likes
13,838
Points
280
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
14,088 13,838 280
Mbali na hilo mchungaji huyo anasema “amani ya nchi haiwezi kupatikana kwa kutumia maguvu na mabavu kwa kuwatishia wananchi.”
Hajui alisemalo.
Hajui kuwa amani haiji ila kwa nja ya UPANGA?
Kazi ya upanga (MAJESHI) ni kuleta amani sio utulivu.Utulivu mtu unatulia mwenyewe ukiwa kwako au ukiwa Sabato kanisani kwako
 
HOMBOY

HOMBOY

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Messages
1,440
Likes
910
Points
280
HOMBOY

HOMBOY

JF-Expert Member
Joined May 16, 2016
1,440 910 280
A
Hajui alisemalo.
Hajui kuwa amani haiji ila kwa nja ya UPANGA?
Kazi ya upanga (MAJESHI) ni kuleta amani sio utulivu.Utulivu mtu unatulia mwenyewe ukiwa kwako au ukiwa Sabato kanisani kwako
si wakati wa mkoloni, katika zama hizi amani huja kwa mzungumzo tatizo wakuu wetu hawataki mazungumzo katika meza moja pale panapokuwa na tatizo. Mchungaji yuko sahihi
 
W

WILLIAM MARCONI

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Messages
2,056
Likes
770
Points
280
W

WILLIAM MARCONI

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2015
2,056 770 280
TANZANIA hakuna amani nchini isipokuwa kuna utulivu, hivi ndivyo anavyosema Bunga Dettu, Mchungaji wa Kanisa la Waadventista (Wasabato) Mtaa wa Dodoma, anaandika Dany Tibason.

Mbali na hilo mchungaji huyo anasema “amani ya nchi haiwezi kupatikana kwa kutumia maguvu na mabavu kwa kuwatishia wananchi.”

Katika mkutano huo amesema, kama wananchi hawataweza kupata nafasi ya kutoa dukuduku zao kwa kunyimwa uhuru, kuna uwezekano wa amani kutoweka.

“Lazima ijulikane wazi kuwa wananchi wanataka kuona wanatendewa haki katika kutoa mawazo yao na kutumia rasilimali walizonazo kwa usawa.

“Lakini kama wananchi wataendelea kuona rasilimali za nchi zinatumiwa na watu wachache huku watu wengu wakiendelea kutaabika, kamwe amani haiwezi kuwepo”amesema Mchungaji.

Abrahman Ahmed, Mwakilishi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmaddiya amesema, jumuiya hiyo ipo kwa ajili ya kukuza uhusiano mzuri kati ya jamii na serikali.

Sambamba na hilo amesema, kazi kubwa ya jumuiya hiyo ni kuhakikisha dini zote zinakuwa na uhusiano mzuri katika kudumisha amani na utulivu sambamba na kuliombea taifa na viongozi wake.
Rasilimali zipi?
 
Forum statistics

Threads 1,238,904
Members 476,226
Posts 29,336,361