Kuna uhusiano gani kati ya ZEC na SMZ?

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
615
Mara baada ya Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar nilitegemea kuwa tume ambayo ndiyo imefuta matokeo hayo isiingiliwe na chombo chochote au umtu yeyote zaidi ya tume kutoa sababu za kina tena zenye maana ambazo zilisababisha kufutwa kwa uchaguzi huo.

Inawezekana ni siri, ila nafikiri huwenda tume iliona mambo ya msingi na kosoro za maana hata hivyo nafikiri tume ingetoa ripoti inayoeleweka ya kasoro zilizojitokeza na hatua zilizochukuliwa kurekebisha kasoro hizo!Pia kwa vyovyote kasoro hizo kuna aliye au waliosababisha ambao nilitegemea tume ingechukuwa hatua ili wale wote waliosababisha hasara yote hii mpaka kurudia uchaguzi wawajibike.

Jambo lingine ambalo sijajua maana yake ni hivi vikao vilivyokuwa vinaendelea kati ya CCM na CUF sijajua vilikuwa ni vya nini, kama serikali SMZ ilikuwa inajua kasoro zilizokuwa zimejitokeza kwa nini kuwe na haja ya kujaribu kujadili na kutafuta muafaka?

Kama kuna taratibu zilizokiuka madili pamoja na taratibu za uchaguzi kwanini majadiliano yawepo, kulikuwa kunajadiliwa na kutafuta muafaka gani? inamaana walikuwa wanabembelezana kurudia uchaguzi au nini? Basi kama ni kurudia uchaguzi tume ingefikiria hoja hizi:-

-Haja ya kuhakiki Daftari la wapiga kura

-Haja ya kujua kama wagombea wote wako tayari au hai kwa kupigiwa kura maana mpaka sasa kuna wagombea ambao wamefukuzwa uanachama wa vyama walivyoviwakilisha sasa Tume iking'ang'ania nafikiri ni kujichanganya.

- CUF wamesema hawako tayari kushiriki uchaguzi, tume ikapeleka jina la mgombea wa CUF, kwa bahati akapigiwa kura za ndiyo wakati yeye mwenyewe keshakataa kushiriki uchaguzi jee tume italazimisha aapishwe kwa nguvu? Huku sio kujichanganya tena? Kuna haja na sababu ya kulazimisha ng'ombe ambaye makataa kunywa maji? Hebu tusubiri kituko hiki
 
Back
Top Bottom