Kuna uhusiano gani kati ya mchana, usiku na upepo?

ZNM

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
1,219
1,280
Jamani naomba kujuzwa kwa kuwa hili nimekuwa nalitafakari na nimekuwa sipati jibu, mimi najishughulisha na shughuli za uchomaji matofari, kazi hii naimudu vema nikiifanya ucku kwa kuwa upepo unakuwa mtulivu kuliko mchana, sasa najiuliza kuna uhusiano gani kitaalamu?
 
Great thinkers naona mnachungulia mnapita!
 
Huu uzi umekosa wataalamu? Google napo ckupata jibu, hii nini maana yake? Only for great thinkers!
 
Naona unatangaza biashara yako ya kuchoma tofali kinamna, ila ngoja sasa niende kwenye mada yako, tofauti ya ya hali ya upepo kati ya mchana na usiku inasababishwa na uwepo wa jua na mwezi.
Mda wa mchana jua huwa linawaka hivyo ardhi inapata moto na kusababisha particle nyingi ardhini kuwa nyepesi hali inayopelekea kupeperushwa kirahisi hivyo mchana kuonekana kama upepo unakuwa mkali kuliko usiku, na kipindi cha usiku ardhi inakuwa imepoa sababu ya uwepo wa mwezi hali inayopelekea particle nyingi ardhini kushikamana kwa kuwa ardhi imepoa hivyo mzunguko wa upepo huonekana ni mdogo sababu particle nyingi hazizunguki angani sababu ya kupoa kwa ardhi.
Note.
Usiku na mchana mzunguko wa upepo huwa sawa ila kinachotofautisha ni uwepo wa jua mchana ambapo ardhi huwa yamoto na kufanya particle nyingi ardhini kupeperushwa kirahisi na usiku uwepo wa mwezi hali inayosababishwa ardhi kupoa hivyo particle nyingi kushikamana kutopeperushwa kirahisi, pia kiasi cha upepo huwa kinaongezeka jinsi unavyokwenda mbali na usawa wa bahari.
 
Mtindo huru ahsante, ila ningekuwa natangaza biashara ningesema napatikana wapi! Umefafanua vema japo nahitaji wengi zaidi wachangie tuone maoni yao!
 
Back
Top Bottom