Kuna tatizo kubwa katika siasa za nchi hii na wala hakuna dalili za kuliondoa!!!!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Mara baada ya kupata uhuru wetu; ilionekana wazi kuwa ingawa tulikuwa wamoja katika tumaini la mafanikio, lakini hata hivyo tulikuwa tumegawanyika kimtizamo kuhusu ni aina gani ya siasa inayotakiwa kuuendesha uchumi wetu. Nilitegemea mara baada ya kuligundua hilo viongozi wetu waliokuwepo wakati ule wangeketi pamoja na wale walionekana kuwa na mawazo tofauti, ili kuutengeneza mustakabari wa pamoja kuhusu kule walikotaka kulipeleka taifa lao changa!!

Kinyume cha hilo viongozi wetu hao kwa sababu zisizo bayana kwetu waliwaona wale wasiokubaliana nao kimawazo kuwa ni maadui wakubwa, huenda kuliko hata wakoloni wenyewe. Huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa tatizo lenyewe lililopelekea mimi kuanzisha mada hii.

Na ni hapo ambapo; kwa kutumia mkono usiyeonekana na wengi mstari wa rangi nyekundu ulichorwa ili kuweka utengo kati ya wenye mawazo sahihi na wale wasio na mawazo sahihi !!
Kwa sababu hiyo jambo hili limekuwa na madhara makubwa katika siasa za nchi hii.

1) ATHARI KWA UPINZANI
Wanasiasa wa upinzani kuwaona wale waliopo madarakani kama makaburu tu! Samahani natumia neno kaburu! kwa sababu sisi tuliokuwepo enzi hizo tulifahamu kuwa haiwezekani kitu chema chochote kitoke kwa makaburu!
Mtazamo huu kwa sehemu kubwa umeweka ukuta kati ya pande mbili hizi. Na kuondoa uwezekano wa mashirikiano ya kweli hata kama ni jambo lenye kuwaletea wananchi wao faida litapingwa tu!

2) ATHARI KWA CHAMA TAWALA
Wanasiasa wa chama tawala wamekuwa na mtazamo hasi kwa wale wenzao wa upinzani hasa pale wanapowaona kama mamluki tu! Wasioweza kuaminika kupewa madaraka ya juu katika uongozi wa nchi hii.
Jambo hili limetengeneza mgogoro mkubwa hapa nchini, ambapo kwa kitambo sasa umeendelea kushika kasi yake ya chini kwa chini mithiri ya moto wa pumba!

Kusema kweli hili kwa kiasi fulani limesababisha kuyumbishwa mno kwa mtazamo wa chama tawala, kutoka kwenye kuwaona maadui watatu ambao ni ujinga, umaskini na maradhi mpaka kwenye kudhani kuwa adui yao mkubwa ni wapinzani wao kisiasa!

Kimsingi hii ndiyo kansa kuu inayoliangamiza taifa hili pamoja na mengine ya kiafrika. Katika karne hii ya kistaarabu napata shida kukiri kuwa sisi waafrika eti bado hatujastaarabika!

Ndugu zangu mniwie radhi kusema hivi; ingawa tunavaa mashati na magauni mazuri lakini roho zetu bado zinaishi katika zama za ujima! Zama ambazo binadamu alikuwa akikutana na binadamu mwenzie madamu hawafahamiani tu walikuwa wanapigana mpaka basi, bila kujari kuwa hawakuwa wamekosana kwa lolote! Hizo zilikuwa zama za ujima!

Leo dunia imestaarabika mno ambapo siku zote wastaarabu ni waungwana!
Ni ajabu mno kwa watu wazima kama kweli tumestaarabika tukaanza kugombana kwa sababu ya kushindwa kutambua utu wetu pamoja na wa wenzetu! Hivi ni kweli tutakaa katika mawazo ya kuwaona wa upinzani au chama tawala kama maadui mpaka lini?

Hivi ni kweli kwamba pasipo kujari itikadi zetu za vyama hatuwezi kukaa chini na kuelezana ukweli kuwa sisi sote ni ndugu?
Na kuanzia hapo tukatengeneza utaratibu tutakaokubaliana sote, naam mfumo wenye kujenga umoja pasi na kupuuza changamoto ya utofauti wa mawazo na hali itakayoondoa migogoro isiyo na tija!

Tunahitaji muafaka wa kitaifa mapema kabla hatujafika kule binadamu aliyekata tamaai anakokimbiliaga!
 
Mimi nimezidharau siasa za ukawa baada ya kujifunga makaratasi mdomoni..nikajiuliza ili iweje?wananchi wamepiga kura wamekuja kulipwa makaratasi?
 
Mie nimeipenda hiyo....

Ndugu zangu mniwie radhi kusema hivi; ingawa tunavaa mashati na magauni mazuri lakini roho zetu bado zinaishi katika zama za ujima! Zama ambazo binadamu alikuwa akikutana na binadamu mwenzie madamu hawafahamiani tu walikuwa wanapigana mpaka basi, bila kujari kuwa hawakuwa wamekosana kwa lolote! Hizo zilikuwa zama za ujima!
Mchokoo kuna somo la kujifunza hapo!!
 
Mara baada ya kupata uhuru wetu; ilionekana wazi kuwa ingawa tulikuwa wamoja katika tumaini la mafanikio, lakini hata hivyo tulikuwa tumegawanyika kimtizamo kuhusu ni aina gani ya siasa inayotakiwa kuuendesha uchumi wetu. Nilitegemea mara baada ya kuligundua hilo viongozi wetu waliokuwepo wakati ule wangeketi pamoja na wale walionekana kuwa na mawazo tofauti, ili kuutengeneza mustakabari wa pamoja kuhusu kule walikotaka kulipeleka taifa lao changa!!

Kinyume cha hilo viongozi wetu hao kwa sababu zisizo bayana kwetu waliwaona wale wasiokubaliana nao kimawazo kuwa ni maadui wakubwa, huenda kuliko hata wakoloni wenyewe. Huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa tatizo lenyewe lililopelekea mimi kuanzisha mada hii.
Na ni hapo ambapo; kwa kutumia mkono usiyeonekana na wengi mstari wa rangi nyekundu ulichorwa ili kuweka utengo kati ya wenye mawazo sahihi na wale wasio na mawazo sahihi !!

Kwa sababu hiyo jambo hili limekuwa na madhara makubwa katika siasa za nchi hii.

1) ADHALI KWA UPINZANI

Wanasiasa wa upinzani kuwaona wale waliopo madarakani kama makaburu tu! Samahani natumia neno kaburu! kwa sababu sisi tuliokuwepo enzi hizo tulifahamu kuwa haiwezekani kitu chema chochote kitoke kwa makaburu!
Mtazamo huu kwa sehemu kubwa umeweka ukuta kati ya pande mbili hizi. Na kuondoa uwezekano wa mashirikiano ya kweli hata kama ni jambo lenye kuwaletea wananchi wao faida litapingwa tu!

2) ADHALI KWA CHAMA TAWALA

Wanasiasa wa chama tawala wamekuwa na mtazamo hasi kwa wale wenzao wa upinzani hasa pale wanapowaona kama mamluki tu! Wasioweza kuaminika kupewa madaraka ya juu katika uongozi wa nchi hii.
Jambo hili limetengeneza mgogoro mkubwa hapa nchini, ambapo kwa kitambo sasa umeendelea kushika kasi yake ya chini kwa chini mithiri ya moto wa pumba!
Kusema kweli hili kwa kiasi fulani limesababisha kuyumbishwa mno kwa mtazamo wa chama tawala, kutoka kwenye kuwaona maadui watatu ambao ni ujinga, umaskini na maradhi mpaka kwenye kudhani kuwa adui yao mkubwa ni wapinzani wao kisiasa!

Kimsingi hii ndiyo kansa kuu inayoliangamiza taifa hili pamoja na mengine ya kiafrika.
Katika karne hii ya kistaarabu napata shida kukiri kuwa sisi waafrika eti bado hatujastaarabika!
Ndugu zangu mniwie radhi kusema hivi; ingawa tunavaa mashati na magauni mazuri lakini roho zetu bado zinaishi katika zama za ujima! Zama ambazo binadamu alikuwa akikutana na binadamu mwenzie madamu hawafahamiani tu walikuwa wanapigana mpaka basi, bila kujari kuwa hawakuwa wamekosana kwa lolote! Hizo zilikuwa zama za ujima!

Leo dunia imestaarabika mno ambapo siku zote wastaarabu ni waungwana!

Ni ajabu mno kwa watu wazima kama kweli tumestaarabika tukaanza kugombana kwa sababu ya kushindwa kutambua utu wetu pamoja na wa wenzetu!
Hivi ni kweli tutakaa katika mawazo ya kuwaona wa upinzani au chama tawala kama maadui mpaka lini?

Hivi ni kweli kwamba pasipo kujari itikadi zetu za vyama hatuwezi kukaa chini na kuelezana ukweli kuwa sisi sote ni ndugu?
Na kuanzia hapo tukatengeneza utaratibu tutakaokubaliana sote, naam mfumo wenye kujenga umoja pasi na kupuuza changamoto ya utofauti wa mawazo na hali itakayoondoa migogoro isiyo na tija!

Tunahitaji muafaka wa kitaifa mapema kabla hatujafika kule binadamu aliyekata tamaai anakokimbiliaga!

Nadhani adhari ulimamisha athari.Ni hoja nzuri ila ninajiuliza kwenye mjadala msipokubaliana nini kinaendelea? Lazima uwepo upande wa kushuka.Nadharia ya win-win katika baadhi ya mambo haiwezekani.Tunaowaita wastaarabu wamefundisha kuwa wanawake na wanaume wapo sawa.Wanaume kwa wanaume waoane kadhalika wanawake.Ni wendawazimu.Wamejadiliana hawajakubaliana.

Upande mmoja ulipopima kuwa hautashinda kwa kuwashawishi wenye hoja tofauti wanatumia risasi,huko mnakoita kwa wastaarabu.Kuna maeneo tumestaarabika kuliko ngozi nyeupe.Tatizo kubwa hatujiamini wala kuamini akili zetu.

Nchi ni kama familia.Kuna mambo watoto wangependa yatangulie,mama anamtazamo tofauti, baba anamtazamo tofauti.Mnaanza mjadala ,mnaumaliza kila mmoja kashikilia upande wake nini kinatokea? Mtoto mwnye adabu husubiri akue awe na uwezo mkubwa zaidi
ya baba na mama yake awathibitishie uwezo wake mkubwa kwa matendo.

Ni tabia ya Lucifer kutaka wote muwe na mamlaka sawa.Haipo popote duniani.Kwa nini Marekani wana mabunge mawili katika nchi moja? na bunge lenye wawakilishi wenye fedha nyingi ndiyo wana maamuzi ya mwisho.Je ndiyo aina ya demokrasia tunayopaswa kuuiga?

Tujadiliane lakini tufikie hitimisho kwa kuangalia upande upi umeshawishi wengi.Waingereza wana msemo "democracy of fools" tujiulize wana maanisha nini na wanamlenga nani.
 
Mimi nimezidharau siasa za ukawa baada ya kujifunga makaratasi mdomoni..nikajiuliza ili iweje?wananchi wamepiga kura wamekuja kulipwa makaratasi?
tatizo TV mmezikutia mjini dunia nzima hiyo kitu ipo
 
Kama hujui hata kutofautisha athari na adhali nadhani wewe mwenyewe unaweza kua na tatizo kubwa kuliko hilo tatizo ulilotaka kuliondoa.
 
Rais keshasema huu Ni wakati kazi nyie bado mnataka kuhubiri siasa tu.

Kawaambieni msubiri miaka mitano iishe nyinyi mkitaka mikutano na maandamano kila Siku wananchi tutalima na kufanya kazi saa ngapi?
 
Kusema rais sio tatizo. tatizo maudhui ya hicho alichokisema inatokana na kifungu gani cha katiba au sheria zetu. kama hakuna ni shida..
 
Back
Top Bottom