Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
Picha halisi ya Deogratius Kisandu na Feki Deogratius Kisandu (Benard Mtorela)
1.Picha ya kwanza ni ya kidato cha pili pale Magu Sekondari januari 1998 yenye Uniform, wa kwanza kushoto ni Deogratius Kisandu(Origino) na wa pili kulia ni Feki Deogratius Kisandu (Benard Mtorela)
2. Picha ya pili ni mwaka 1997 mjini magu siku za wikendi, mwenye kofia ni Deogratius Kisandu (origino) na Mwenye Fulana ya bluu ni Feki Deogratius Kisandu (Benard Mtorela).
Natoa taarifa hii kwa watanzania ili wajue kabisa kuna watu wanatumia majina ya watu kwa maslahi ya kuchafua majina ya wengine.
Bwana Bernad nilikuwa naye Magu sekondari(eveninig class) na tulikuwa darasa moja kuanzia kidato cha kwanza mwaka 1997 na mwaka 1998 mwezi wa pili mimi Deogratius Kisandu niliacha shule na kujiunga na Utawa wa Ndugu wadogo wa afrika Morogoro ambapo awali ilitakiwa niende shirika la SFS LububuTabora japo ilishindikana. Tukiwa Kidato cha pili mimi nilienda utawani na mwaka 1999 mwezi April nirirejea nyumbani kahama na kujiunga na Kishimba sekondari (evening class) kwa kuanza tena kidato cha kwanza mpaka mwaka 2002 nilipohitimu kidato cha nne.
Nimejiendeleza mpaka kufikia hatua ya kuwa Shahada ya juu na kuwa katika mfumo wa ajira rasmi.
Chakushangaza, kumbe nilipoondoka Magu sekondari mwaka 1998 huyu Bwana Benard aliacha kutumia jina lake na kuendeleza jina langu(Deogratius Kisandu), wenzake walimzuia sana lakini hakusikia na taarifa zinasema kuwa aliambiwa kuwa Deogratius Kisandu ameshaga kufa siku nyingi, naye yeye akiwa amefikia hatua ya juu kwa kutumia jina langu, na mimi Deogratius Kisandu nilipoanza kuinuka kisiasa na kimziki watu walianza kumhoji juu ya uhusiano wa jina Deogratius Kisandu, aliwadanganya watu kuwa mimi ndio nimeiba jina bila kujua kama kuna watu wanamfahamu vizuri. amekuwa akihangaika kuwahonga baadhi ya ndugu zangu ili wasimshitaki ambao mpaka sasa hao ndugu sijawajua.
Bw. Benard kwa mala ya mwisho alikuwa mfanyakazi DSM kwa jina langu na sasa inasadikika yupo NMB Magu-Mwanza akitumia jina langu na watu wamekuwa wakimsihi kwenda kuapa lakini anajificha.
Natoa angalizo kuwa aache mara moja kuchezea jina langu, sijamlazimisha kulisomea wakati mimi niliishia njiani na kwenda Utawani. Na sasa Bw. Benard anatumia jina langu mpaka kwa watoto wake na anaoogopa kumwambia mke wake ukweli wa mambo, naomba Usalama wa Taifa na watu wote wa intelejensia kunisaidia kwa hili kwani jina langu Limedhalilishwa.
Imefikia hatua huyu FAKE Deogratius Kisandu amekuwa akiwasiliana na viongozi wakubwa na kusema yeye ndio mimi, kitu ambacho kimesababisha mateso sana kwangu na ndugu zangu kutishwa juu ya kusema ukweli huo, sasa nmeinuka nasema LIWALO na LIWE. Nitatoa picha yake na yangu wakati tunasoma magu tukiwa kidato cha pili mwanzoni.
DEOGRATIUS NALIMI KISANDU.