Kuna mtego Iran anaingia pasipo kujua

mtetezi12

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
23
Reaction score
116
Kuna mtego ambao Iran anaingia pasipo kujua

Ushabiki wekeni pembeni tujiulize kabisa kama Marekani na Israel wana uwezo wa kujua siri za ndani ya Iran yaani nina maana kujua wapi viongozi wa juu wa Iran walipo na kuwaua. Je, washindwe kujua uwezo kamili wa kivita wa Iran?

Je kama walijua Iran ni tishio kwao kwanini wali attack Iran ?

Je kwanini wanawekeza nguvu zao nyingi katika kujitetea na kuonyesha dunia kuwa wanaonea ? Kama umefatilia vizuri vita hivi zaidi upande wa Israel wamekuwa wakionyesha huruma kuwa wanaonewa na Iran inashambulia makazi ya watu,wao wana shambulia vituo vya kijeshi.

Kwanini wanashindwa kutangaza vita kamili zidi ya Iran?

Ukijiuliza maswali yote haya utagundua kuna hesabu za mbali zinapigwa hapa ambazo matokeo yake yatakuja kujulikana hapo mbeleni kidogo tuombe uzima tu​
 
Kila mtu kaona iran kachangiwa na mataifa mawili , inatosha kabisa kusema Israel peke yake bila marekani ni mchumba tu kwa iranView attachment 3556273
Yani Israel kawekwa rehani, marekani anapigana vita na iran katika ardhi yake. Irani harushi chochote Marekani, kila kitu kitamalizikia palepale.

Yani kama isra3l kakodisha geto watu wakapigane miti
 
Unadhani Muajemi hayajui hayo unayoyahisi wewe? Anachosumbuka nacho miaka nenda rudi ni lile kundi dogo la makabila ya kusini ambayo ni almost 20% ya population ya hao ambao kwa kiasi kikubwa ndio wauza taarifa za Muajemi kwa Israel ila pamoja na yote Muajemi kwa intelijensia ni mwamba kupitiliza. Achana na stereo type tuliyolishwa miaka nenda rudi ya Israel na Marekani kuhusu intelijensia zao.
 
Kwenye mambo ya intelijensia Israel yuko mbele sana, huwezi mcompare ni Iran
 
Huyu binti ni mpiganaji au ameenda kuvaa gwanda na kupiga picha tu?
Inatosha kusema hiyo pic ni AI kwasababu hakuna binti wa umri huo wa kufikia cheo hiko cha general katika jeshi la Iran. Mpaka ufikie cheo hiko inakubidi uwe umepitia ngazi mbalimbali na zinazochukua muda mrefu mpaka kufikia miaka zaidi ya 30-40.
 
Inatosha kusema hiyo pic ni AI kwasababu hakuna binti wa umri huo wa kufikia cheo hiko cha general katika jeshi la Iran. Mpaka ufikie cheo hiko inakubidi uwe umepitia ngazi mbalimbali na zinazochukua muda mrefu mpaka kufikia miaka zaidi ya 30-40.
Yeah
 
Hizo hesabu walishindwa kuzipiga wakati wanachezea kichapo kule Vietnam na Afghanistan hadi wakafungasha virago kwa aibu?

Ukweli ni kwamba Iran anao uwezo mkubwa wa teknolojia ya zana za kivita ndiyo maana anajipogia popote atakapo ndani ya ardhi ya Israel pamoja na kuzichakaza kambi zote za Marekani mashariki ya kati.

Kumbuka Marekani na Israel wana mifumo imara sana ya ulinzi wa anga lakini umeshindwa kuzuia makombora ya Iran. Hadi hapo bado unaibeza nguvu ya Iran?

Iran anazitandika nchi zaidi ya kumi kwa mpigo na kwa shabaha halisi bado unapigwa propaganda za miaka ya 80?
 
Inatosha kusema hiyo pic ni AI kwasababu hakuna binti wa umri huo wa kufikia cheo hiko cha general katika jeshi la Iran. Mpaka ufikie cheo hiko inakubidi uwe umepitia ngazi mbalimbali na zinazochukua muda mrefu mpaka kufikia miaka zaidi ya 30-40.
Inawezekana akawa ni mtoto wa mkubwa akapandishwa vyeo ambavyo hastaili, ila vitani wanaenda wale waliotakiwa kuwa na vyeo staili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…