Kuna mahala Nyerere alikosea

NANCA

Member
Joined
Jun 23, 2023
Posts
92
Reaction score
100
Hivi Tanganyika iko wapi? Mbona Zanzibar tunaiona. Rais wa Tanganyika yuko wapi? Mbona wa Zanzibar tunamjua. Bendera ya Tanganyika iko wapi? Mbona ya Zanzibar ipo. Na katiba je ya Tanganyika maana ya Zanzibar ipo.

Nadhani kuna mahala Nyerere alikosea hesabu zake au alitaka sifa kwamba yeye ni mtu mwema sana hata akafanya harakaharaka akaingizwa mkenge na karume bila kujijua.

Alichotakiwa kufanya Nyerere ni kumwambia karume kua baada ya mapinduzi haya, tunaifuta Zanzibar na historia yake na itakua mkoa wa Tanganyika na ww bwana karume utakua waziri mkuu wa Tanganyika na mimi ni Rais na watanganyika watakua huru kutembelea popote ktk nchi yao na Zanzibar kuanzia sasa itaitwa Singida au n.k. Kama hilo lingefanyika leo hii kelele zisingekuepo.
 
Mimi Huwa naamini hivyo Zanzibar ni mkoa wa wavuvi ,,wakina Mwinyi kwao ni bara.FULL STOP.
 
Tanganyika aliingia kwenye ndoa na mwanamke asiyempenda . Hivyo Tanganyika anaingia kwenye gharama zisizo za lazima kulinda muungano usiokuwa na tija kwake yeye (Tanganyika).
 
Too lake to cry
 
Elimu ya history inahitajika hapa kujua chanzo cha muungano, pia Elimu ya civics inahitajika kuwafundisha watu muungano wetu ni muungano wa aina gani!.

P
 
Elimu ya history inahitajika hapa kujua chanzo cha muungano, pia Elimu ya civics inahitajika kuwafundisha watu muungano wetu ni muungano wa aina gani!.

P
Ni serikali tatu au serikali moja....hizi nyingine ni utapeli
 
Ya nini yote hayo ?????

Kama Zanzibar ingefanywa kama Singida Karume angepewa Uwaziri Mkuu kwa nini ??????????????

Singida au Tanga, kama Florida au Arizona, kwenye Muungano wa Marekani, hawajawahi kutoa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika, Jaji Mkuu, nothing! Na hatujawahi kusikia malalamiko na stress kutoka Singida wala Florida, kwa sababu Singida na Florida hawana ahadi kwamba watatoa Waziri Mkuu. Singida ni Mkoa, Florida ni jimbo. Period! End of story!

Kwa formula yako wewe bado tungekuwa na stress za Muungano!

Zanzibar ni ndogo kuliko Uyui. Zanzibar inaingia Sikonge mara 12. Wapewe Uwaziri Mkuu kwa lipi la zaidi walilonalo ????????
 
Miaka 60 ya Muungano kila upande bado una kinyongo.
Katiba mpya iamue aina nyingine ya Muungano, serikali moja au laa serikali tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…