Kuna Magufuli na kuna CCM..!

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Wakuu nimetafakari hili jambo baada ya juzi kwa bahati mbaya kujikuta nipo katikati ya viongozi wa serikali wa mitaa na wanachama wa Ccm eneo la Chanika Jimbo la Ukonga Dar es salaam waliokuwa wamekutana kwa ajili ya kupanga mikakati ya kampeni za uchaguzi jimbo la Ukonga.

Nilichokigundua Ccm ni ileile na watu ni wale wale wenye mawazo yaleyale na unafiki uleule.!
Ni kweli tulio wengi. Tunavutiwa na uongozi wa Mh Rais John Pombe Magufuli..
lakini msingi wa wanachama wa Ccm na wale wanaokibeba hiki chama huku chini kwa kweli ni matatizo makubwa na ni wazi kwa aina ya watu walioko huku hupati shida kujua kwanini Chadema wanawachukia sana CCM..

Ccm imejaza watu wanafiki wao pia wanalifahamu hili vema, aina ya uongozi wao kuanzia ngazi ya shina kuelekea Tawi na kadharika uovu ulio ndani yao bila shaka hakuna asiye ujua wale wanaoichukia Ccm wanaichukua kwa sabbu ya watu hawa.

Nami niwe wazi huenda mlio ndani Ya CCM hamjui na hasa viongozi wa juu, lakini ikiwa
Hii ndio Ccm muisemayo hakika kizazi hiki hakitapita CCM mtaangushwa vibaya sana, labda kama itatokea mmeacha UNAFIKI, HILA,RUSHWA NA UZANDIKI..

vinginevyo lazima mjue mtaweza kuwadanganya na kuwahadaa watu fulani kwa wakati fulani ila sio rahisi kuwahadaa watu wote wakati wote.

Mlioshiriki kile kikao pale Chanika mnafahamu vema mliyokuwa mnajadili na mlichopeana.
Wasalaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawewe ulipewe??

Sent using Jamii Forums mobile app
Badirikeni mkuu zama zimebadirika Watanzania hawa wa leo sio kama wale walio warithisha hicho chama.
Hawa wanawaangalia na wanajua madhaifu yenu msifikiri ni wajinga wana uelewa wa kutosha. Wanaipenda Ccm kutokana na historia yake lakini ikiwa watu wenyewe walio kwenye chama ni aina yenu.

Muda utaongoea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Kweli CCM Siku Moja haitokuwepo
Kwa Kuwa Mwenyezimungu Pekee ndie wa Milele Ila kuota Hawa Nyumbu wana Medula
Oblangata ya kuitoa CCM ni kujikebehi Ki fikra
 
Ni Kweli CCM Siku Moja haitokuwepo
Kwa Kuwa Mwenyezimungu Pekee ndie wa Milele Ila kuota Hawa Nyumbu wana Medula
Oblangata ya kuitoa CCM ni kujikebehi Ki fikra
No watakao iondoa CCM sio hawa unao waona Chadema.. leo la hasha wataoindoa CCM madarakani ni Wana Ccm wenyewe walio ndani ya CCM.

(Huwezi kumkata kipepeo kwa panga mpaka utakapo jua njia zake)

Kuna watu wapo CCM na hawapendezwi na huu upumbavu unaofanyika ndani ya CCM.. wewe pia unalijua hilo mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sasa CCM wakitoana Madarakani si itakuwa Kama Kenya walishangilia Kuondoka Kwa KANU Na Sasa wana Uhuru Kenyata
 

Sijaelewa unaposema Chadema wanaichukia CCM. Wao wanafanye tofauti. Unadhani kama vita vya Ndani Vitatokea chanzo ni nani. Soma mitandao ya wanachadema wabunge nk. Ni taarabu ni Majungu. Chadema ya Slaa haipo tena. So ndo unataka wao washike dola. Are you serious. Ona ajenda Leo ya Makonda Hakuna sera tena. Hakuna mwelekeo. You have to give yourself an Identity before you parade your own ideas to others. Find your identity.
 
Umesomeka mkuu Nchi hii tunayoishi tumeazimwa tu na watoto wetu. Hatuna umri mrefu wa zaidi ya miaka 50 mbele yetu swala la msingi endapo sisi tulirithi uovu huu kutoka kwa walio tutangulia je tunawaachia pia watoto wetu?

Tunafahamu uozo na kiburi cha watu ambao hawana Elimu wala ujuzi walivyokabidhiwa nafasi nyeti za maamuzi katika serikali na Taifa letu kwa ujumla kwa kisingizio cha siasa,
Tunafahamu yaliyokuwepo pale B.O.T , Bandari, TRA, na hata kwenye mifumo yetu ya Ulinzi na Usalama, hatukatai kama siasa ingekuwa imetumika kuwapata watu sahihi wanaostahili kuzipata nafasi hizo.
Nani asiyejua kuhusu vimemo na maagizo yalivyokuwa yanatumika kutoa maamuzi..?

Inakera unapodhani yale mambo yameisha na sasa Chama kinauelekeo mpya kama ambavyo unawasikia viongozi wakuu wa chama wakijinasibu, lakini ukitumbukia humu ndani ndimo unapojua kile kinachoendelea.

Yamkini hata Chadem wako hivyo kama ambavyo tunawafahamu, lakini je tofauti yetu basi itakuwa ni ipi kama wao wanafanya kama CCM na CCM wanafanya kama CHADEMA?

mkuu si jambo jema kuwarithisha watoto wa wenzio kilio cha baba yao.! Wao wanaweza wasilie lakini wakakujibu kwa aina mpya kuondoa machungu yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…