Habari zenu wanajamvi...nashindwa kumuelewa huyu mpenz wangu ni yule mtu ambaye ikitokea mmekorofishana atakuongelea maneno machafu sana yan hauamin kama yametoka katk kinywa chake,ivi karibuni umetokea ugomvi kidogo amenitamkia maneno ambayo kila nikimuona napatwa na hasira sana anajidai kuomba msamaha,je huyu n mtu naeweza kuishi nae kwa amani pindi tutakapofunga ndoa?
Thanx kwa ushauri ila hapo kwenye KAKA weka DADA na hapo kwenye MWANAMKE weka MWANAMMEKaka huyo mwanamke anaonekana hana heshima kabisa yaani bf wake afu anakutukana as if kama mmeokotana bar au disco, my friend think twice about it... over!
Mimi ni KEWewe ni ke au me?
Nikuambie ukweli bila kukufariji; utaweza kuishi nae ktk ndoa ila hutamfurahia, utakuwa mtu wa kumvumilia tu kwa huo mdomo wake usio na break. Swali - utaweza kumvumiliGa kwa kiasi hicho, bila kikomo, yaani maisha yako yote? Jibu lako obvious ni hapana maana tayari hapo amekutibua sana hadi ukimwona unapata hasira, hivyo ni wazi huwezi kumvumilia huyo.
Ushauri mchungu hapo ni kuwa huwezi kuishi naye ktk ndoa ukapata furaha haijalishi hata kama anayo mazuri mengi sana anayokufanyia, kwa hii thread yako umeonyesha hilo huwezi kulivumilia, amua mapema uepuke kujitafutia stress for the rest of your life. Wapo watu wanaweza kuvumilia maneno machafu lakini naona sio wewe! Shukuru huyo hajaweza kukuficha, amejionesha waziwazi, ungekuwa tayari kwenye ndoa ingekuwa balaa!
Anadai kuna future na anakua akinielezea pale nakosea ili kunirekebsha kwasababu ananipenda,binafsi najiuliza mbona ye ananiudhi ila cjawah hata cku moja kumtamkia maneno machafu anadai n hasira,nkamwambia hasira zimemfanya atoe yale aliyonayo moyon kwa cku nyngMosi, Uliwahi kumwuliza hilo swali? Alijibu nini?
Pili, una bahati haya yamewatokea hamjafunga ndoa...sepa...
Mapenzi ya tamthilia tena!!?
Nashukuru kwa ushaur umenena vyemaKuhitilafiana katika mapenzi na hata kupandisha jazba si jambo la ajabu lakini ni vizuri kuwa waangalifu ili kujua ni maneno gani yanayostahili kutotamkwa ili usije kutamka matusi ya nguoni yakasababisha penzi kuingia dosari kubwa na hata kuvunjika. Kama mwenzio ana tabia ya kutoa maneno machafu/matusi ya nguoni nawe huwezi kuyastahamili basi kama hatakuwa tayari kubadilika na kuachana na lugha chafu ni vizuri kufanya maamuzi magumu haraka.
Khaaa!PLL, future ipo kabisa!! Kuna tamthilia moja imeanza hivi karibuni Star TV(kama upo TZ) inaitwa MaraClara! Kwahiyo ndoa itawepo na itakuwa kama ya Gerry na Suzan....kama upo TZ, nakushauri fuatilia hiyo tamthilia ili ikupe maamuzi sahihi....weekend saa 3 usiku; ijumaa na jnne ni saa 3.30 usiku.