Kuna binti amenipenda sana ingawa ni mchumba wa mtu na wamezaa mtoto mmoja na mumewe anampenda sana

kali popote

JF-Expert Member
May 3, 2017
394
281
Habari za asubuhi JF,

Nianze kwa kusema kwa ufupi sana. Mimi ni mwenyeji wa Arusha katika pita pita zangu nilikutana na binti kwa muonekana ni mzuri na mrembo sana nikampenda akanipenda na kuanza mahusiano ya kimapenzi.

Muda kupita nikajagundua yule binti kumbe alikuwa na mume wake na wameshazaa na mtoto mmoja ingawa la mtoto alishawahi niambia anae ila la mume hakuwahi niambia kwani alinambia mume wake aliezaa nae wameshaachana hivyo yupo single na kumbe ni muongo na ukweli ni walikuwa wakiishi pamoja.

Baada ya kuligundua hilo niliendelea kuwa nae ingawaje kwa kijihadhari sana nikajua huyu ni wakupita tuu na mwishoe kila mtu afuate yake, siku nenda rudi yule binti alipata post ya kwenda masomoni mkoa flani hapa Tanzania kwa ajili ya kujiendeleza na elimu ya ualimu. Binti tuliagana akaondoka kwenda masomoni na hapo hapo haikuchukua muda na mimi nikapangiwaga huko huko mkoa alipoenda yeye kwani nilisha omba maombi ya shahada na nilikubaliwa na kuondoka.

Baada ya kufika huko nilijiamulia mwenyewe yule binti nisimtafute na nimuache kwani asingeweza kunifaa kwanza kanidanganya ile mwanzo na pia anae mtu tayari na kuhusu umri alinipita miaka miwili mimi ninae 27 na yeye anae 29.

Hivyo niliamua kutafuta mwanamke mwingine ambae nilikuwa mkoa huo ingawa nae alikuwa ni mwanafunzi wa ngazi ya cheti cha nursing na mortuary tulianza mahusiano na muda haukupita huyu binti akashika ujauzito wangu, kiukweli niliwaza sana ukizingatia nilikuja kusoma huku lakin nilipiga moyo konde nikamuhaidi kuilea hiyo mimba mpaka atakapo jifungua.

Kimbembe ni yule binti wa mwanzo sasa baada ya kujua kuna binti nipo nae na nimempa ujauzito aliumia sana tena sana na alicho amua yule binti nikutoa msimamo wake wa dhati kwamba pamoja na yote hayo hawezi kuniacha hata kama yametoka hayo maana amenipenda sana na alikubali hata kumuacha mumeo wa kwanza aliezaa nae kisa mimi hapa hivyo ni ngumu na hawezi kuniacha na alisema bora afe kuliko anikose mimi.

Nimalize kwa kusema huyo binti niliempa mimba ameshajifungua na mtoto wa kiume na ana miezi saba sasa na ananipenda sana pia. Shida ipo kwa yule binti kwanza alienizid umri kwani nae bado ananipenda sana na hayupo tayari kuniacha amesema.

Naombeni ushauri wenu wa dhati wana JF kwani nipo katika wakati magumu sana
hata sielewi nifanyaje.
 
Asa unachouliza hapo ni nini mkuu?....kweli huna chakufanya hapo?...kweli?!...like seriously?!
 
Huyo uliezaa nae ndio anauzito huyo aliemuacha mumew hajielew katema bigjii kwa karanga ya kuoncheshwa ebu fanya maamuz yakiume watoto wamitaani wanaongezeka kila itwaaho leo mtoto apate shida kisa umalaya wako jitambue we cyo mtoto ndio maana ukazalisha mtu
 
Inaonekana ww ni Fundi kitandani maana wanaume wengi wanapiga piga tu juu juu hafu wanawaacha wenzao kwenye wakati mgumu hivyo akipata mwanaume anayejua mambo lazima amkimbie mume wake, hivyo punguza ufundi mkuu
 
Tatizo letu wanaume tamaa!

Kama uliamua kumuacha kinacho kurudisha nini?
Shida tunazaa na wanawake wasio machaguo yetu, inapelekea akipata ujauzito inakuwa kama ndio wa kuishi nae.

Hali ya kuwa ulikuwa kwa ajili ya kukatia ukakasi, mi nakushauri piga moyo konde acha tamaa chukua uamuzi wa kukaa na huyo uliyezaa nae sababu yule unayesema anakupenda hawezi kukuacha ni una mtamani tu na najua leo hii ukalee mtoto wa watu wakati una wako umemuacha itakuwa sio rahisi tena ukizngatia ulidanganywa.
 
Tatizo letu wanaume tamaa!

Kama uliamua kumuacha kinacho kurudisha nini?
Shida tunazaa na wanawake wasio machaguo yetu, inapelekea akipata ujauzito inakuwa kama ndio wa kuishi nae.

Hali ya kuwa ulikuwa kwa ajili ya kukatia ukakasi, mi nakushauri piga moyo konde acha tamaa chukua uamuzi wa kukaa na huyo uliyezaa nae sababu yule unayesema anakupenda hawezi kukuacha ni una mtamani tu na najua leo hii ukalee mtoto wa watu wakati una wako umemuacha itakuwa sio rahisi tena ukizngatia ulidanganywa.
Ahsante mkuu ushauri mzuri sana nimeupenda
 
kama una akili achana na mke wa mtu anakwambia anakupenda huenda kwa sababu hawelewani vizuri na mme wake...harafu ni kwambie ukweli tu kuchukua mke wa Mtu ni kutafuta kifo cha mapema. Wew umeshapata aliye wako achana na Mzinzi huyo atakuharibia Maisha yako....MARK MY WORD
Ahsante mkuu nimeelewa
 
Back
Top Bottom