Salaam.
Leo nimeona iwe vyema kuwaletea maajabu ya huyu Kijana, anaitwa Mbuyu "Junior" Twite. Kuna facts za Ajabu sana kuhusu huyu kijana tangu aliposaidiwa na Agent wake "Aden Rage" kutua pale mitaa ya Jangwani.
Nina kila sababu kusema kuwa huyu Kijana hajutii hata mara moja kutua kwa wanajangwani. Maana kuna Maajabu kadhaa aliyo sababisha tangu atue pale Jangwani.
Maajabu 5:
Tangu Mbuyu "Junior" Twite atue Jangwani mnamo 31/08/2012.
1. Simba haijawahi beba Ubingwa wa LigiKuu Tanzania. Kwa lugha nyingine Mbuyu Twite hajawahi kuiona Klabu hiyo yenye makazi yake pale Msimbazi (Matopeni) wakibebwa Ubingwa.
Ila siwezi kubisha kuwa njia pekee ambayo huenda alitumia ni kuingia Google na kupakua (download) picha za simba akibeba ubingwa misimu ya nyuma kabla ya 2012 kwa lengo la kuzitazama tu.
2. Tangu atue Jangwani amebeba Ubingwa wa VPL mara nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote yule wa simba ndani ya Miaka 16 iliyopita.
VPL:- 2012/13 - 2014/15 - 2015/16.
Azam Sports Federation Cup - 2015.
3. Tangu Mbuyu Twite asaini Jangwani Klabu ya Simba haijawahi kushiriki michuano yeyote mikubwa nje ya Tanzania.... Namzungumzia (CAF)
4. Tangu asaini Jangwani Klabu ya Simba imebadilisha walimu (Makocha) wasio pungua 5.
5. Tangu ajiunge Jangwani amecheza Dar Derby 9. Ambapo amepoteza mechi moja (1) tu dhidi ya Simba....kwa bao moja bila.
Shukrani sana Mbuyu Twite.
Leo tunakuaga rasmi pale uwanja wa Uhuru kwa mechi ya kirafiki dhidi ya JKU Zanzibar.
Ama kweli Uwepo wako Jangwani ulikuwa mwiba mkali mno ndani ya maisha ya Mashabiki wa Msimbazi. Tutakukumbuka sana. Haswa kwa haya Maumivu uliyosababisha kwa Warani zetu.
....