Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
KUMUELIMISHA MJINGA ALIYEBAHATIKA KUFIKA ELIMU YA JUU,(KWA KUKARIRI) NI NGUMU SANA
Inakuwa ngumu kwa sababu kwanza hakuna past papers za kukariri na kunukuu,wala hakuna mwalimu wa kumuuliza,inabidi ujiongeze mwenyewe kwa kutumia elimu uliyonayo kulielewa jambo lililopo mbele yako,ikiwa ni pamoja na kutafuta facts zinazo husiana nalo,ili uweze kutoa suluhuhisho
Sasa hebu tuangalie kazi hii ilivyo ngumu katika hoja za msingi na majibu yake kwa kuangalia suala la madini ,ni dhahiri, kweli kazi ipo
1.Jamani mikataba hii ya madini haifai kuifanya siri wenzetu wachache watashirikiana kutuibia
Jibu:Mikataba hii ni siri wapinzani msilete chokochoko,kama vipi tupige kura,wanaosema ipite waseme ndiyo ,Ndiyoooooo
2.Jamani huu mkataba unaoruhusu mchanga kupelekwa nje bila kujua ndani una kiasi gani cha madini si mzuri tunapoteza pato kubwa la Taifa bila kujijua
Jibu:Wapinzani mnaionea wivu serikali ya ccm jinsi inavyotekeleza vizuri ilani na sera za kisasa za mageuzi na uwekezaji,hamjui kwamba sasa dunia ipo pamoja(utandawazi)na kituo chetu cha kukuza uwekezaji kimeshika nafasi ya kwanza duniani mwaka huu na kupata nishani ya juu kabisa ,msituhangaishe tupige kura ,wanaosema serikali ya ccm iendelee na nia yake nzuri ya kushirikiana na wawekezaji ili kuweza kuikomboa nchi yetu kiuchumi,kuruhusu mchanga uendelee kupelekwa nje,waseme ndiyo, Ndiyoooo, imepitaaaa
3.Jamani huu mkataba unaowapa wawekezaji dhahabu yetu bure na wao kutakiwa kutupatia asilimia 3 tu ya fedha zote watakazopata katika mauzo (mrahaba)ni wa hovyo,ni wizi wa mchana na haufai,yaani wao wachukue 97% sisi watuachie mashimo,magonjwa na umaskini?
Jibu:Tatizo lenu wapinzani ni kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali ya ccm,uwezo huo hamna na serikali ya ccm itaendelea kuwaletea wananchi wake maendeleo kwa kuhakikisha dhahabu hiyo inaendelea kuwa ya wawekezaji na serikali kuendelea kupokea mrahaba wa asilimia 3%,waheshimiwa wabunge mkiongozwa na wabunge makini wa CCM,katika msimu uliopita pato la taifa limekua kwa asilimia 6.3,mfumuko wa bei umedhibitiwa na kuendelea kuwa asilimia 12 na tunategemea utapungua kufikia asilimia 8 katika nusu ya pili ya mwaka ujao wa fedha,wakati huo huo mipango yetu mizuri iliyomo kwenye vision 2015, Mkurabitita, Mkukuta, Mmem na Mmes ikiendelea,tunampongeza sana Rais wetu Makini na chama chetu makini,naomba wabunge mtuunge mkono, mnaoafiki semeni ndiyo,Ndiyooooo
Baada ya miaka 17 kazii inanza upya wale wote waliopitisha kwa kishindo Ndiyooooo,wanasema mchanga una madini mengi kuliko declaration,tunauzuia hautoki tunaunda tume,wanaambiwa serikali ya ccm ni makini (sic!)haiwezi kukubaliana na wizi huu unaotokana na mikataba mibovu,mchanga wetu hautoki,wanasema tena Ndiyoooooo, wezi wakubwa hawa wasituchezee (my god baada ya miaka 17?)
Wanashauriwa tena:Jamani kwa mujibu wa mikataba ya aibu na wizi mliyo tuingiza,fuateni utaratibu wa kisheria tujitoe katika mikataba hii mibovu ikiwa ni pamoja na kujitoa katika makubaliano ya kimataifa tuliyo jifunga kuwalinda wawekezaji na hao walio weka sahihi mikataba hii mibovu
Jibu:Wapinzani mnawatetea wawekezaji,tunajua mnapewa hela,hivi karibuni tutawaumbua,na nyie mnae tafuta tafuta taarifa kule tunawajua karibu tutawashughulikia
Tobaa yaani lugha gongana kweli kweli,sijui ni Hapa kazi tu au Kazi tunayo,nimechooka kabisa na nchi hii,yenye wasomi wasioelimika,wanaotaka tumpongeze aliyeua mtoto wetu kwa kuwa amekubali kugharamia gharama zote za msiba?
mimi nitakuwa wa mwisho kuwaelewa ,naomba mnisamehe naweza kuwa mjinga zaidi kwa kuwa mimi ni zao la wajinga walio toa madini yetu bure,mnayo kila sababu ya kunisamehe,wajinga hawanyongwi huelimishwa,msiniteke wala kunipeleka mlipo mpeleka Yericko Nyerere mtapoteza nguvu zenu bure, mawazo yangu hayatafutika,ndiyo maana nimeona niyaseme kidogo hapa,kwa kweli kazi tunayo(hapa kazi tu!)
Ni mimi mmoja wenu mjinga wa Tanzania