Kumtenga Manji na walevi wa mpira ni kazi ngumu

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,423
13,935
Mpira wa miguu soka unaongoza duniani ikiwemo Tanzania kwa kuwa na mashabiki wengi hadi kwenye ngazi ya vitongoji. Wapenzi wa mpira wa miguu wanapata arosto kama wakishindwa kuziona au kusikiliza mechi za timu zao zinapocheza, sawasawa na walevi wengine wanapozikosa dawa zao. Wapo mashabiki wanaopoteza maisha kwenye matukio ya timu zao zinapofungwa na wengine wanafanya uharibifu na uhalifu mkubwa wanapodhani kuwa timu zao zimeonewa uwanjani au hata kufangwa kihalali.

Timu inapotafuta ushindi haijali ni nani na kwanamna gani ushindi huo utapatikana. Pamoja na ubaguzi walionao wazungu dhidi ya watu wa mataifa mengine lakini linapofika suala la ushindi wa timu yao hawatajali rangi, utaifa, dini wala tabia ya kocha, mchezaji na mfadhili wa timu.

Tanzania Simba na Yanga zimezoa watu wooote mijini na vijijini wa tabaka tofauti, na kwa bahati mbaya timu hizi mbili pamoja na kuwa na mashabiki wengi hivo lakini zinatengemea ufadhali wa watu binafsi. Mafanikio yao yanategemea na utayari na uwezo wa mfadhili wao kuweza kununua na kuwalipa makocha na wachezaji wazuri, wakati mwingine hata "kununua" baadhi ya mechi. Hivyo basi wale wote wenye ulevi wa mpira (ambao ni wengi sana) watampenda mfadhali, kocha na mchezaji wao anayesababisha timu ishinde bila kujiuliza maswali (unconditionally) mengi na vilevile watamchukia kupita kiasi mfadhili, kocha, mchezaji au mtu yeyote yule ambaye atasababisha timu yao ishindwe. Hii ni fact.

Kwasasa timu ya Yanga ni mwendo mdundo, inaongoza ligi na inakabiliwa na mashindano mengi makubwa ya kimataifa, unaonaje hapo kwa mashabiki wa Yanga...?

Sheria, busara na hekima vyote vitumike. Sisi sote tumsaidie Rais wetu katika kuliunganisha taifa na watanzania katika dhamira yake njema ya kuwavusha watanzania kwenda kule anakokuona yeye kuwa kunatufaa sisi wote.
 
Taifa lenye umoja ni lile lenye kufuata sheria. Rule of law. Acha sheria tuliyokubaliana nayo ifanye kazi.
 
Taifa lenye umoja ni lile lenye kufuata sheria. Rule of law. Acha sheria tuliyokubaliana nayo ifanye kazi.
tusitenganishe sheria, busara na hekima. Sheria ipo lakini kuna watu hawakunyongwa hadi leo ingawa sheria imewatia hatiani. Watu waliomuua Yesu walitekeleza sheria na kuiweka busara na hekima kando.
 
Back
Top Bottom