Kumkubali kwa hiari

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,190
Kumkubali mtu, inaweza kuelezwa ni kumpokea, kumheshimu, Kumkaribisha, Kumpa nafasi pengine sawa sawa na yako. Kumkubali rafiki au mwenza ni tendo linalotegemewa kuwa la hiari, sio la lazima. Katika mahusiano mengi yawe ya kirafiki, kiuchumba, au katika kazi, unapompata mtu, bado ni mgeni kwako,hujajua uwezo na udhaifu wake, n.k Ni wakati ambao unapaswa uwe na mshikamano wa akili na moyo wako kuhakikisha unamkubali mtu aliyesahihi kwako tena kwa hiari yako mwenyewe! Kumkubali yule unaefikiri atakufaa katika hitaji lako,liwe ni la urafiki, uchumba, ndoa au kazi, ni kukubali changamoto zinahitaji udhibiti binafsi (self control), Kumkubali kwa hiari ni kukubali yafuatayo;
....
HAKI YAKE YA KUWA TOFAUTI NA WEWE
Kuna watu wanaingia katika mahusiano kwa imani kuwa, yeye atamwendesha aliye mbele yake apendavyo. Anafikiri atabeba jukumu la kumwelekeza tu, aache kazi zake, uwezo wake, na pengine utu wake muda wote awepo pale unapomhitaji. Ukifikiri hivyo unakosea, huyo aliyepo mbele yako si wewe! Ni yeye. Kubali anapotoa maoni yake, Kubali anapochelewa, Kubali anapochukia, Kubali anapofurahia. Hapa ndipo kumkubali kwa hiari kunapoleta shida. Hasa unapotarajia urafiki wenu, uchumba wenu au ndoa yenu itakunufaisha wewe zaidi kuliko yeye.
....
KUBALI UDHAIFU WAKO
Kuna watu wanahitaji juhudi binafsi kujikubali wao. Pasipo kujikubali ulivyo haitakuwa rahisi kuwakubali wengine. Kuna watu hawakubali sura zao, maumbile yao, hasira zao, viburi vyao, kutojua kwao, majivuno yao n.k Usipokubali udhaifu wako umekataa kubadilika. Na usijikubali basi hutawakubali wengine kwa hiari maana pale wasipokidhi matarajio yako kwao utajificha katika udhaifu wako ili uwaone wao ndio wenye makosa!
....
SOTE TUNATOKA KATIKA HISTORIA YENYE MAKOSA
Kukubali unaempenda kwa hiari maana yake ni kukubali kuwa anatoka katika historia yake yenye vikwazo fulani. Anaesema barabara ya maisha yake ilikuwa imenyooka toka azaliwe mpaka alipo, basi asubiri wakati unakuja ambapo atajua maisha si barabara nyoofu, ina maudhi, mikosi, majaribu, chuki, kuachwa, kuumizwa n.k ambako kutaathiri sehemu fulani ya urafiki, uchumba, kazi au ndoa yenu.
...
KUMKUBALI KWA HIARI, ni jambo linalohitaji uvumilivu sana. Linahitaji uangalifu. Si kila kukubali kunaleta kukubalika, unapoona hukubaliki usiulazimishe moyo wako, kuna kituo kingine kitakupa your pair
 
uko sahihi kabisa mkuu hasa kwa hapa ambapo nafikiri tulio wengi tunakosea.


HAKI YAKE YA KUWA TOFAUTI NA WEWE
Kuna watu wanaingia katika mahusiano kwa imani kuwa, yeye atamwendesha aliye mbele yake apendavyo. Anafikiri atabeba jukumu la kumwelekeza tu, aache kazi zake, uwezo wake, na pengine utu wake muda wote awepo pale unapomhitaji. Ukifikiri hivyo unakosea, huyo aliyepo mbele yako si wewe! Ni yeye. Kubali anapotoa maoni yake, Kubali anapochelewa, Kubali anapochukia, Kubali anapofurahia. Hapa ndipo kumkubali kwa hiari kunapoleta shida. Hasa unapotarajia urafiki wenu, uchumba wenu au ndoa yenu itakunufaisha wewe zaidi kuliko yeye.
 

^^
utashangaa mtu anataka uwe yeye!!! Is it possible?
^^
 
Blue G, unajua ulivunja promise lakini?
najua mamito but please naomba nichukue fursa hii kukuomba msamaha,am so sory and please be patient please give me some more time ni lazima nitimize ahadi hata kama ni kwa kuchelewa.
 
Ila me nafikiri wanaume ndo hawajui kukubali kwa hiari. Anakukuta uko hivi mkishaingia kwenye uhusiano antaka kukubadilisha uwe vile....tena anataka mabadiliko ndani ya siku moja....kitu ambacho hakiwezekani.
Ataanza kufuatilia historia yako.....ataiponda bila kujali ilikuwaje hadi ukapitia hayo uliyoyapitia. Huwa najiuliza kama wanataka wakamilifu si watafute malaika? Hakuna binadamu aliyekamilika, tujifunze kuwavumilia wengine na kukubali madhaifu yao....kwani hatuwezi kupata watu ambao tutaendana nao asilimia mia, lazima kuna sehemu tutasigana na hapo ndipo uvumilivu unahitajika kwa kukubali madhaifu yetu na ya wenza wetu.
 

^^
Hili ni tatizo la kila upande Kim nana nachoweza kusema ni kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wa kumkubali mwanaume kuliko wanaume. If you find yourself not ready for changes that's not love for you
^^
 
Last edited by a moderator:

Ur right
 
Tatizo la upendo/mapenzi mara nyingi humtoa mmoja wa wahusika uelewa au wote wawili kiasi cha kutokufikiria logically.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…