Kumekucha CCM, aliyepigwa rungu na Ndugai ateuliwa Ukuu wa Wilaya

Ukana Shilungo

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
3,041
2,422
Dr. Joseph Chilongani alipigwa rungu na NDUGAI akazimia wakati wa kura za maoni jimbo la Kongwa mkoani Dodoma.

Amepewa UDC Meatu, kapewa zawadi kupoza makali ya maumivu ya rungu alilokuwa amepigwa. Hongera ndugu Chilongani Joseph.

1438155428671.jpg


Cc :Simiyu Yetu, lizaboni, faiza fox, shindu NAMWAKA.
 
Joseph chilongani alipigwa rungu na NDUGAI, kuteuliwa, akazimia wakati wa kura za maoni. Amepewa UDC Meatu, kapewa zawadi kupoza makali ya Maumivu ya rungu alilokuwa amepigwa. Hongera ndugu chilongani Joseph. Cc :Simiyu Yetu, lizaboni, faiza fox, shindu NAMWAKA.
Mkuu tupatie kwanza cv zake kabla hatujachangia kiundani
 
Ukuu wa wilaya kwa wanataaluma wakati mwingne ni majanga tu. Sasa huyu alikuwa daktari tena mkubwa, anaacha mshahara na utumishi anaingia kwenye kazi za uteuzi alafu mara kesho kutwa kafukuzwa au kuachwa tu bila maelezo. Hapo ndyo watu wengne wanaanza kujuta kwanini nilikubali uteuzi na kuacha kazi yangu nzuuuri?
 
Acha akale kiyoyozi. Afu kuna uzi kama huu uliletwa jana ukaunganishwa na ule wa uteuzi wa wakuu wa wilaya.
So mleta mada hapa tegemea chochote...
 
Duuu! Bongo noma kumbe kupigwa na mtu maarufu kinalipa pia kupiga mtu maarufu nako ni dili maana mheshimiwa Makonda si alimpiga mzee Warioba baadae akateuliwa kuwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni na sasa mkuu wa mkoa wa Dar ea salaam.

Miaka ya nyuma pia aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Tarime marehemu kwa sasa Pascal Mabiti aliwahi kumpiga mwandishi wa habari lakini baadae alipandishwa ngazi kuwa mkuu wa mkoa wa Singida,

Pia Magesa Mulongo alipokuwa mkuu wa wilaya ya Bukombe aliwahi kuwapiga na kuwaharibia vifaa vya kazi waandishi wawili wa habari baadae akahamishiwa Bagamoyo na muda si mrefu akateuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha.

Ama kweli hii ndo Bongo ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.
 
Mkuu Ukana Shilungo!
Wakati unampongeza Chilongani kwa kuteuliwa kuwa DC mkumbushe arudi kwa Sangoma ategue Zongo alilompiga Ndugai Kama inawezekana ili aokoe maisha yake. Ila kama Kinyamkera kimekwenda alijojo basi tumpe pole Ndugai ashauriwe kula mbegu kwani hachomoki hata akikaa India. Chezea Afrika ndumba!
Ndugai hachomoki! Maskini Job kirungu cha mponza! Halafu pengine ni Kitenngo kinamshughulikia na sio Dr.Majimarefu!
 
Ukuu wa wilaya kwa wanataaluma wakati mwingne ni majanga tu. Sasa huyu alikuwa daktari tena mkubwa, anaacha mshahara na utumishi anaingia kwenye kazi za uteuzi alafu mara kesho kutwa kafukuzwa au kuachwa tu bila maelezo. Hapo ndyo watu wengne wanaanza kujuta kwanini nilikubali uteuzi na kuacha kazi yangu nzuuuri?

Awamu hii wataalamu wengi sana wakiwemo wahadhiri wa vyuo vikuu wametolewa vyuoni na kupewa ajira za kisiasa.

Sina hakika kama wanaoteuwa wanaangalia madhara yatakayotokea huko wanakowatoa wataalamu!
 
Duuh nimefurahi sana aisee! Yani kumbe siku hizi mtu kutoa / kupokea kichapo kunaongeza CV ? Kweli ktk TZ maajabu hayataisha kamwe !
 
Back
Top Bottom