Kumchagua Lissu mwenyekiti TLS ni kuzika lengo la kuanzishwa kwake

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862

Wanabodi,

Kumekuwepo na mjadala wa hapa na pale tokea bwana Tundu Lissu kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa chama cha sheria Tanganyika, binafsi niweke wazi tu kuwa mimi Tume ya Katiba ni miongoni mwa wale wanaopinga kwa nguvu zote huyu bwana kuchaguliwa kuongoza chama chenye jukumu muhimu kama kile chenye malengo mazuri kwa Watanzania wote. Natoa wito kwa Serikali, na idara zake zote kutumia nguvu zao zote kuzuia jaribio baya kabisa kuwahi kutokea katika fani ya sheria Tanzania.

Chama cha sheria Tanganyika ni nini? kilianzishwaje ? na Malengo yake ni yepi?
Chama cha sheria Tanganyika kilianzishwa mwaka 1954 na sheria ya Bunge sura namba 307, Chama hiki ndiyo chama pekee cha mawakili na wanasheria kinachotambuliwa kisheria. Miongoni mwa majukumu ya chama hicho ni kuwatetea wananchi katika mambo ya kisheria ili waweze kupata haki zao, pia chama hiki ina jukumu muhimu la kuishauri serikali katika mambo mbali mbali yahusuyo sheria


Je ni kweli kwamba chama hiki hakikosoi serikali hivyo kumuhitaji Lissu?

Nimeshitushwa sana na kauli za baadhi ya watu kuwa chama hiki kilikosa Meno hivyo kumuhitaji mtu kama Lissu, nitaweka baadhi ya mambo ambayo chama hiki kiliyafanya ambayo nina hakika hayawezi kuwa yaliipendeza serikali. Mosi, ni chama hiki hiki kwa kushirikiana na Mtikila pamoja na kituo cha haki za binaadamu kilifungua shauri katika mahakama ya afrika mashariki dhidi ya Serikali kudai haki ya mgombea huru asiyefungamana na chama, Pili, june 2016, chama hiki kilitoa kauli kulaani vikali kauli iliyotolewa na naibu kamishna wa pilisi zanziba iliyowatisha wanasheria kuwa kama watawatetea wahalifu mahakamani na wao watakamatwa, Lakini chama hiki pia kilipoona Bunge la katika haliendi sawa na maoni ya wananchi yamewekwa kando kiliiomba mahakama kuu tanzania iwaruhusu kufungua shauri lenye mwelekeo wa Kupinga Bunge la Katiba. Kwa kuwapa taarifa tu ni kwamba ni chama hiki ndicho kilipendekeza mkuu wa polisi asiteuliwe na Raisi na kuwe na tume maalumu ya uteuzi kwa kuwa kwa kuchaguliwa kwake na Rais anakosa nguvu katika kudhibiti na kutekeleza kazi zake. Mifano ipo mingi, isipokuwa nimeweka michache ili kuonyesha kuwa upotoshaji unaoendelea sasa sio wa kuachiwa. Kwa mifano hiyo ni dhahiri kwamba si kweli Chama hiki hakitimizi wajibu wake wa kuishauri na kuipinga serikali isipokuwa wao huyafanya haya kisheria na sio kimihemko.


Je ni kweli kwamba Serikali haitaki wanasiasa wa upinzani kuongoza chama hiki?

Kuna dhana imeanza kutengenezwa kwamba, wanaopinga Lissu kuchaguliwa wanapinga upinzani kuongoza chama hicho, wengi wenye mtazamo huu wamefika hadi kuhusisha chama hiki na chama tawala cha CCM jambo ambalo halina ukweli wowote, kwa kuweka mfano tu ni kwamba mwaka 2013-2014 Peter Kibatala ambaye anafahamika kabisa ni miongoni mwa viongozi wa CHADEMA alikuwa ndiye Makamu mwenyekiti wa TLS, kama wanaompinga Lissu wanampinga kwa chama chake kwanini basi wasingefanya hivyo hivyo kwa Kibatala ambaye ndiye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama?
Kwa mfano huu basi hoja ya chama cha Lissu na yeye kuwa mpinzahi haina mashiko.

Kwanini Lissu Hafai kuongoza chama cha sheria Tanganyika?
Lissu, pamoja na kukiri kwangu kuwa ni miongoni mwa wanasheria mahiri katika Taifa hili, amekosa sifa muhimu ya kuwa na busara na hekima, Elimu pekee haitoshi mtu kuweza kuongoza kama utakosa hekima na busara, Lissu ni mwanaharakati, Lissu hawezi kuzuia mdomo wake, Lissu hawezi kucontrol taharuki na hasira zake, lakini kubwa zaidi ni kuwa Lissu hawezi kutenganisha sheria na siasa na atapeleka u-anasiasa wake kwenye chama hivyo kupoteza mwelekeo wa chama. Lissu atabadili mwelekeo wa chama na kuanza kushughulika ma mambo ya kisiasa, na kesi za kisiasa kuliko kesi za kijamii zisizo za kisiasa ambao ziko nyingi zaidi, ushahidi wa hili ni tazama idadi ya kesi ambazo Lissu anazishughulikia kwa sasa mahakamani 95% ya kesi zote ni zenye mwelekeo wa kisiasa au kukashifu serikali au viongozi wa juu wa serikali ambazo kwa mbali zina mwelekeo wa kisiasa.

Ripoti ya miezi sita ya Chama cha wanaseria wa Tanganyika ya kuanzia January 2013 hadi july 2013, inaonyesha kuwa chama kilitoa jumla ya usaidizi wa kisheria 132, kwa kiwango kikubwa usaidizi huo ulihusu mambo yanayohusu na kuachishwa kazi bila kufuata taratibu, migogoro ya ardhi, Madai yatokanayo na ajali, unyanyasaji wa kijinsia na unyanyapaa. Hakuna katika mashauri hayo, chama kilitoa kwa mambo ya kisiasa. Tunapofikilia kumkabidhi chama mtu ambaye katika maisha yake amekuwa akitoa usaidizi kwa mambo yahusuyo siasa tu ni kwamba mambo mengine yahusuyo jamii yataachwa hivyo wananchi kukosa haki yao ya kisheria

Kwa muktadha huo basi, Lissu Hafai na anakwenda kuharibu chama kwa kukiweka mbali na jamii na serikali ambayo chama kinaihitaji kufanikisha mambo yake mbali mbali. Lissu anakwenda kuhari malengo muhimu ya chama. Lissu Hafai Hafai.


Mwisho
Nimalize tu kwa kusema, wanachama wa chama cha wanasheria Tanganyika ambao mna jukumu kubwa sana mbele yenu, msikie sauti hii, sauti inayowataka muendelee kufanya kazi zenu kwa uadilifu bila kujiingiza katika siasa, Lissu anafahamika, Lissu ni Mwanaharakati, Mkimchagua Lissu mtakuwa mmefanya kosa kubwa la kihistoria na historia itakuja kuwahukumu.

Kwa upande wa serikali na hasa Rais wa JMT ndugu Magufuli, tuseme inatosha sasa, mtu ambaye anakesha kutoa lunga za kejeli kwako na kwa serikali yako, lugha za kuudhi leo anapewa jukumu kubwa mbele yako?...Hapana, Tumia uwezo wako, na ushawishi wako kuhakikisha Lissu hashindi katika kinyang'anyiro hichi. Uwezo unao, Nguvu unazo..sina hakika na nia.


Ni hayo tu.

Tume ya Katiba.



Update 09-03-2017

Kazi ya kuhakikisha Lissu hachaguliwi kuwa kiongozi wa Chama cha wanasheria imekamilika.

Nichukue fursa hii kuwashukuru sana wanasheria waliokubali wito na kushiriki katika vikao mbali mbali kujadili hatari inayoikinyemea chama.
Kwa taarifa tu kwa wana JF ni kwamba zaidi ya 60% ya wapiga kura wa chama cha wanasheria wameridhia kuwa Lissu hafai, na wameahidi kutokumchagua.

Nawashukuru sana watu wote waliotoa maoni yao juu ya kuzuia jaribio baya kabisa kwenye taaluma ya sheria, nawashukuru wale waliowezesha hili kwa hali na mali.

Asante

Update 18/03/2017

Kura zinaendelea kupigwa, matokeo yameshatangazwa.

Siku njema
 
Akili za kushikiwa ndivyo zilivyo! Akiwa kada wa MACCM katika nafasi hiyo hakuna tatizo ila akishika mtu wa chadema ni kosa kubwa sana! Peleka ujuha wako pale Lumumba.
Mkuu usome vizuri mada, swala sio chama cha lissu kama ni chama Peter Kibatala amewahi kuwa makamu wa raisi wa chama 2013, na anafahamika kuwa ni kiongozi wa chadema.
 
Jaji kugombea kwa tiketi ya ccm sawa. Mwanajeshi kupewa cheo ccm sawa. General wa jeshi kugombea ubunge kwa kupitia ccm sawa.
Lissu kutofaa ni Mawazo yako. Wajumbe ndio wataamua. Usitumie nguvu kubwa kupigana na ukuta.
 
Tunahitaji ukakasi zaidi TLS. Si ukondoo.

I grant you that Tundu Lissu may not be the most diplomatic lawyer there is, but he is not a diplomat.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom