Itakumbukwa, kwenye mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia Juni 8, 1990 kule Italia, Argentina, mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia kwa wakati huo, walibaki midomo wazi wasiamini kilichotokea. Ilukuwa ni kisa cha mende aliyeangusha kabati.Kule Italia mwaka 1990 tuliona jinsi Argentina walivyoweweseka uwanjani mbele ya Cameroon.
Pamoja na kushuhudia beki wetu Andre Kana Biyik akitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika ya 62 ya mchezo kwa kumpiga daruga Claudio Cannigia na si hapo tu, Benjamini Massing, naye akapigwa kadi nyekundu baada ya kumkaba kwa nguvu Diego Maradona karibu katika muda wote alipokuwa uwanjani kiasi cha Maradona kuonekana kupotea kabisa uwanjani. Ili kumpa nafasi Maradona kupumua, na hivyo kuwabeba mabingwa watetezi Argentina, refa ikafika mahali akachomoa kadi nyekundu kwa Benjamin Massing.
Hata hivyo, pamoja na kadi hizo nyekundu, Cameroon ikafanikiwa kupata bao la kuongoza kwa bao maridhiwa la kichwa la Omam Biyik. Argentina kama kabati, likawa limeangushwa na mende!
Mmoja wa watu watakaoishi wasisahau kipigo kile ni Diego Armando Maradona. Na kwa maneno yake mwenyewe baada ya mpira kumalizika, Maradona alisikika akitamka; " Si Cameroon iliyoshinda, bali ni sisi tuliopoteza mchezo!"