Mwanangu mmoja ndio alikua ananiandikia hizo barua zangu maana mimi limuandiko langu la kizembe lilikua
ukishapewa barua yako unaificha kati kati ya daftari,sasa siku moja nina mawenge nimekusanya daftari ndani lina barua
na madftari monitor kashayachukua kayapeleka staff yapo mezani yanasubiriwa kusahishwa,aseeeeeee ile siku nilikaa shule mpk watu wakanishangaaa, school bus imekuja nimeenda jificha toilet gari ikaondoka nikaachwa Hapo nipo natafuta taiming niingie ofisini nikachukue daftari langu nitoe ile barua.
wakati naranda randa shule mlinzi akaniona akaniita "wewe kuja huku" akaanza nitwanga maswali kwann sijaenda nyumbani,nikamdanganya nipo tuition akaniachia.
kuhangaika kote huko sikufanikiwa pata upenyo wa kuingia staff,matokeo yake kesho yake class niligeuka mfano kwa wanafunzi wote na kesi yangu ilifika hadi school baraza nlikomaga mimi jamani, barua hizi pputtuuuuuuu