Ni kweli kauli za dada huyo ni tata, mimi aliwahi kuniambia kuwa NSSF haihusiki na ucheleweshwaji wa malipo hivyo kama kina malalamiko yapelekwe shirika la Posta wao hawahusiki! Chakujiuliza wastaafu wanamkataba gani na Posta? Ukweli ni kwamba kuna unyanyasaji mkubwa kwenye malipo ya mwezi kwa wastaafu.Siku ya tarehe 3/6/2018 baadhi ya wazee walienda makao makuu ya NSSF kufuatilia pension ya mwezi wa tano ambao baadhi yao hawajapewa hadi sasa kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.
Wazee wale wakionekana kuchoka na kukata tamaa, mmoja wa wale akina dada aliyekuwa anawahudumia pale makao makuu ghorofa ya 10 nadhani aliona kwake ni usumbufu akatoa kauli ya kuwaambia wale wazee kuwa 'hata hivyo hizi pension tunazowapa ni msaada tu NSSF inatoa kwenu hamjastahili kuzipata'.
Wazee wale walipigwa na butwaa kwa hiyo kauli na mmoja kati ya wale wazee alishindwa kujizuia na akamwambia yule dada kuwa hata yeye Mungu akimjalia atafikia umri kama wao na vilevile Mwenyezi Mungu akipenda anaweza asifike.
Wazee wale waliambiwa kuacha namba za simu warudi nyumbani watafahamishwa.Sasa kwa jambo hili la wazee kukosa pension na majibu tata ya kiwango hiki tunadhani NSSF kuna shida.
Ni vyema NSSF wakalitolea kauli hili swala kwa ujumla wake kwani watu wameanza kuwa na tafsiri mbaya.Sasa mifuko ikishaunganishwa na wanachama wakawa wengi zaidi hali itakuwaje?
Corrected3/6/2018 hii si ni siku ya jumapili? au NSSF wanafanya kazi siku saba za wiki samahani mkuu hebu tueleweshe kabla hatujatoa lawama
Huyo dada yupo ofisi gani nani namba ngapi , au tutajie alivyo ili ashughulikiwe kama wengine wanaotumia madaraka vibaya na sheria ifuate mkondo.Ni kweli kauri za dada huyo ni tata, mimi aliwahi kuniambia kuwa NSSF haihusiki na ucheleweshwaji wa malipo hivyo kama kina malalamiko yapelekwe shirika la Posta wao hawahusiki! Chakujiuliza wastaafu wanamkataba gani na Posta? Ukweli ni kwamba kuna unyanyasaji mkubwa kwenye malipo ya mwezi kwa wastaafu.
Anyway najua huwezi kumshughulikia ila yupo ghorofa ya kumi chumba cha kwanza kushoto zilipo mashine za photocopy. Tatizo mfuko hauna msimamizi na hauhangaikii matatizo ya wastaafu wahusika wamejikita kwenye kugawana pesa zisizo na mwenyewe.Huyo dada yupo ofisi gani nani namba ngapi , au tutajie alivyo ili ashughulikiwe kama wengine wanaotumia madaraka vibaya na sheria ifuate mkondo.
Ni tarehe 1/6/2018.Already corrected.3/6/2018 hii si ni siku ya jumapili? au NSSF wanafanya kazi siku saba za wiki samahani mkuu hebu tueleweshe kabla hatujatoa lawama
Huwezi kuamini hasa pale anapomjibu majibu yaliyopinda mtu ambaye ni makamo ya babu yake kule kijijini.Anajisikia na anajiona yupo 'on top of everything'.Hakika nssf ni kaa la moto kwa wastaafu.Wazee wale ni 'helpless' hata wanapojibiwa majibu ya ovyo hubaki kimya na kubaki kumshuru Mungu tu.Wale wafanyakazi wa makao makuu nssf, especially wadada wana majibu ya shombo sijapata ona.
Mmh!Ni kweli kauli za dada huyo ni tata, mimi aliwahi kuniambia kuwa NSSF haihusiki na ucheleweshwaji wa malipo hivyo kama kina malalamiko yapelekwe shirika la Posta wao hawahusiki! Chakujiuliza wastaafu wanamkataba gani na Posta? Ukweli ni kwamba kuna unyanyasaji mkubwa kwenye malipo ya mwezi kwa wastaafu.