Kumbe matapeli bado wapo

Kumbe matapeli bado wapo

lutajangurwa

Senior Member
Joined
Sep 21, 2019
Posts
126
Reaction score
172
Hawa Jamaica bado wapo kwa sana. Hii ni jana tu. Kama siyo msichana wa dukani kushtuka, ningepoteza laki nne hivi hivi. TCRA bado wana homework

Screenshot_20220926-212948_Phone.jpg
Screenshot_20220926-213243_Phone.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_20220926-213243_Phone.jpg
    Screenshot_20220926-213243_Phone.jpg
    31.2 KB · Views: 7
ndo wanatapelije?
Screenshot ya kwanza, ni namba ambayo alitumia kutuma txt kwa mfanyakazi wa dukani. Alijitambulisha kama mke wangu. Alimuuliza maswali kuhusu mauzo na hali ya wateja. Mwisho alitaka kujua kuna cash kiasi gani.

Baada ya kuambiwa kuna laki nne (taarifa ya kumdanganya), alitaka atumiwe laki tatu na themanini.

Screenshot ya pili, ni namba ambayo tapeli alitaka itumwe pesa.

Namba zote tukizipiga, wanapokea lakini hawaongei.
 
Sasa ndio wamefanyaje
Wameingia mitini. Swala nnalojiuliza, ilikuwaje namba ya tapeli, ionekane kwenye phonebook ya mfanyakazi wangu, kama Mama BOSS, wakati mke wangu hana namba hiyo?. Kwa ufupi, kwenye phonebook ya simu hiyo, Mama BOSS anaonekana kuwa na namba mbili. Ya tapeli na ya kwake halali. Ajabu!
 
Utakuta watu kama hao nao wakitapeliwa na kuibiwa wanaumia na kulalamika na kulaani na kutukana.

Utakuta majambazi nao kwenye nyumba zao wameweka fensi milango na madirisha ya chuma
 
Kwakweli
 
TCRA. ACHA NICHEKE MIE, niliwaperekea kesi yenye ushahidi toka kampuni ya simu kwa wizi niliofanyiwa, niliambulia manyoya tupu, nilikampigia waziri nae akaomba vielelezo nikampa napo nikaambilia manyoya! Nimeamua kukaa kimya baada ya kuhisi ile kauli ya urefu wa kamba ! Kama huna kamba basi mwachie mungu, maana yy huwapiga makansa🤣🤣
 
Wameingia mitini. Swala nnalojiuliza, ilikuwaje namba ya tapeli, ionekane kwenye phonebook ya mfanyakazi wangu, kama Mama BOSS, wakati mke wangu hana namba hiyo?. Kwa ufupi, kwenye phonebook ya simu hiyo, Mama BOSS anaonekana kuwa na namba mbili. Ya tapeli na ya kwake halali. Ajabu!
Kuna uwezekano huyo mtu anayewafanyia hua mchezo anawafaham vizuri kabisa ,
IPO hivi kilichotokea hapo ni mtu kachukua simu ya huyo sijui dada wa kazi na kusave hayo majina na kutaka atumiwe pesa kua yeye ni boss kumbe ni boss fake

Aepuke kuwapa watu Simu yake hovyo hovyo
 
Inawezekana mkuu. Asante kwa ushauri
 
Wameingia mitini. Swala nnalojiuliza, ilikuwaje namba ya tapeli, ionekane kwenye phonebook ya mfanyakazi wangu, kama Mama BOSS, wakati mke wangu hana namba hiyo?. Kwa ufupi, kwenye phonebook ya simu hiyo, Mama BOSS anaonekana kuwa na namba mbili. Ya tapeli na ya kwake halali. Ajabu!
mkuu mwambie huyoo binti wako wa dukani aache kuwapa watu simu ovyoo maana inaonekana kuna mtu wa karibu sana ame fanya hilo jambo sio kwamba ni matapeli wa mbali
 
Hatari. Kikulacho ki nguoni mwako
 
Dada wako wakazi atakuwa anakibwana chake au marafiki zake wakike ndio wamemfanyia ujinga huo muulize Taratibu tuu
 
Back
Top Bottom