incredible terminator
JF-Expert Member
- Aug 1, 2016
- 2,229
- 3,525
Tunaaambiwa kuwa uyaone nami leo nilochoambiwa na huyu mwamba kimenifanya nijiulize mara mbilimbili.
Kuna mshkaji wangu tumemaliza nae chuo mshikaji akawa anajishughulisha na kuuza mitumba jamaa kasota sana kwenye mitumba huku mi mwanae nipo mtaani na kibodaboda changu. Kwa kipindi hiko maisha yangu bodaboda ila nilikuwa na unafuu kuliko yeye sasa cha ajabu mwana life limebadilika gafla mwana anapiga pesa na maisha yake yamebadilika ghafla sana hadi ikabidi nimuulize mwana kafanyeje maana ni gafla sana.
Ndo mwana kanambia ukweli kuwa alienda kwa mtaalam sehemu akapewa ndagu ya biashara, kidogo kuskia neno ndagu nilishtuka sana maana mwana kwao napajua na sijawai ona tatzo lolote pia mwana ni mwanangu wa karibu ila sijawai ona mapichapicha yoyote kwake wala masharti yoyote yakunistua ndo nikaulizia mwana ndagu hiyo ndo ikoje?
Mwana kanambia alipewa kitu cha kutembea nacho na sharti lake ni asje kuzini akiwa nacho wala asije kufanya ugomvi wala dhuruma akiwa nacho, pia aliambiwa apende watu, asiwe mbaguzi na awe mcheshi mda wote. Na akiona wana wanapata shida awasaidie na zile furaha watu wanazopata kutoka kwake ndo utajiri wenyewe,
Pia mwana alisema pesa zake au mkono wake usije kudhiriki kutoa mtu dam au uhai, mfano ikitokea akahonga watu pesa wamdhuru mtu hapo ndo kavunja masharti, au ikitokea yeye apige mtu kwa mkono wake hapo ndo kavunja masharti.
Na nilivopata shauku ya kujua hiko kitu maana kwa fkra za kawaida nilidhani labda ni mijoka au kitu cha kutisha sana ila mwana alinioneshea kadude kadogo tu kama kagoroli kakashonea kwenye kacha na anakavaa kama urembo tu kwenye cheni ya shingoni hata huwezi kidhania kama ni kitu cha maajabu.
Sasa hapa nimekuja kwenu wadau ivi kweli kuna ndagu zenye masharti rahisi kama haya ya wema au mwana kanipanga.