Fundi selemala alipewa oda ya kuchonga jeneza kwenye msiba ambao ulikuwa niwakusafirisha kwenda kuzika mkoani. Alijitahidi kuchonga jeneza faster lakini ikashindikana akakamilisha kazi usiku. Alipomaliza akawapigia simu wafiwa kuwa jeneza liko tayari nao wakamwambia kodisha gari ulilete tutakuja kulipa. Kwa kuwa alikuwa na kigari chake akaamua kulipakia kuelekea eneo la tukio. Umbali kidogo tu kabla hajafika kwenye msiba gari yake ikaishiwa mafuta hivyo ikabidi aamue kujitwisha jeneza ili alifikishe maana hapakuwa mbali na kwenye msiba. Akiwa anatembea na jeneza kichwani ghafla wakatokea wagambo wakiwa kwenye doria, jamaa akawaza faster, "hawa jamaa watanisumbua na sina cha kuwapa hivyo akaendelea kwenda mbele kama vile hajawaona. Kama kawaida ya wagambo wakamstopisha jamaa na kuanza kumhoji na mazungumzo yakawa hivi:
Mgambo: Wewe unaelekea wapi na jeneza usiku wote huu tena peke yako?
Fundi selemala: Nilifariki ndugu zangu wakanizika makaburi ya Kinondoni ila sijapapenda nimeamua kuhamia Mbezi karibu na nyumbani kwangu, au nyie mnanishaurije? Nibaki Kinondoni wakati kwangu ni Mbezi hapo tu?
Kabla hata kauli hiyo haijaisha wagambo wote walikuwa wameshapotelea kwenye vumbi speed mbaya!