Kulipa Kodi ni Wajibu - Kodi Maradufu ni Udhalimu

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Nchi inatakiwa kuwa na kodi sawia (fair taxation) na siyo kodi ya dhuluma. Pale ambapo kiwango cha kodi kinakuwa kikubwa kuzidi wastani wa pato la mwanafamilia mmoja, hiyo ni kodi dhulumati. Mathalani katika familia, Baba pekee yake ndiyo mwenye kipato, na kipato chake ni shilingi 1,000,000 kwa mwezi, halafu kodi inakuwa ni shilingi laki 2. Ina maana familia inabakia na shilingi laki 8. Kama huyu Baba ana mke na watoto 4 tegemezi, wastani wa pato la kila mwanafamilia linakuwa shilingi 133,333. Kodi ya shilingi laki 2 inakuwa dhulumati maana inazidi wastani wa pato la kila mwanafamilia. Serikali inakuwa imeamua kuwadhulumu watu wake inaodai kila siku kuwa inawatetea.

Watanzania sasa hivi tupo katika dhuluma kubwa kwa kupitia kodi.

Kila mmoja anahitajika kulipa kodi kwaajili ya maendeleo lakini siyo kuwa na kodi mrundikano kwa mapato yale yale. Mfanyakazi amelipwa mshahara, amekatwa kodi ya mapato (PAYE). Pesa yake imepelekwa benki. Akiigusa tu ATM, anakatwa VAT. Akichukua hela ile ile akamtumia mtoto wake kwa MPESA, Airtel Money, Tigo Pesa au Ezy Money anakatwa tena VAT, iliyobakia akisema alipie DSTV au Azam TV kwa njia ya simu analipishwa VAT, akisema anunue shati ataenda kulipa tena VAT.

Mimi nilidhani wabunge wangeweza kuonesha uwajibikaji wao kwa waliowachagua, kwa kumfahamisha Waziri wa Fedha na serikali kuwa anayechukua hela kwenye ATM machine, haendi kutafuna zile noti, lazima atafanya manunuzi ambayo tayari yatakuwa na VAT. Anayetuma hela kwa njia ya simu au anayechukua, haendi kuzitafuna zile noti, ni lazima atafanya manunuzi mahali fulani, atalipa VAT. Lakini sikusikia wabunge wakiwatetea watu wao. Sauti zao zilisikika zaidi waliposema kiinua mgongo chao nacho kikatwe kodi.

Watawala wetu, na hasa Rais, atambue kuwa:
1) Mrundikano wa kodi na kuwa na kodi mnyororo siyo uhakika wa kuongeza mapato ya serikali. 2) Kodi dhalimu hujenga chuki dhidi ya serikali, watawala na hata mamlaka za kodi
3) Kodi dhalimu huua biashara, na mwishowe hupunguza mapato ya serikali
4) Kodi dhalimu huua/huzuia uwekezaji
5) Kodi dhalimu hudumaza ukuaji wa uchumi
6) Njia sahihi ya kuongeza mapato ni kuongeza shughuli za kiuchumi na kuzisaidia zile zilizopo ili ziweze kukua lakini siyo kuongeza idadi ya kodi au kumlipisha mlipa kodi yule yule maradufu kwa mapato yale yale

Serikali ijifunze kwa mataifa kama Dubai, ni namna gani kodi ndogo na chache zimeweza kukuza uchumi wao na kisha kuongeza mapato ya serikali. Tanzania tuna nafasi nzuri sana ya kukuza uchumi wetu, kuongeza ukubwa wa biashara na mapato ya watu binafsi na serikali, kama tutaamua kutumia zaidi akili na weledi kuliko nguvu. Kodi ndogo, chache na rafiki zina uwezo wa kuifanya Dar Salaam kuwa soko la jumla na rejareja ambalo wananchi wa mataifa kama Zambia, Malawi, Rwanda, DRC, Zimbabwe, Uganda wangekuwa wanakuja kununua na kuuza.

UCHUMI SIYO NGUVU BALI NI WEREVU.

Watanzania tusidanganyike kuwa ni matajiri. Sisi ni maskini sana ambao tunatakiwa tutumie akili na kila fursa iliyopo ili tupate maendeleo. Utajiri mkubwa ni akili na wala siyo idadi ya simba na fisi tulio nao Serengeti. Utajiri ni akili wala siyo idadi ya maziwa na mito tuliyo nayo. Utajiri ni akili na siyo almasi, dhahabu au gas, ambavyo vyote tunavyo. Ukiwa na akili, simba anakuwa ni rasilimali ya kuweza kukuingizia pesa. Ukiwa mjinga uwepo wa simba inakuwa ni laana maana unaweza kuawawa na kuliwa na huyo simba.

Watanzania ni maskini sana maana hata kuwatunza simba, fisi, na tembo ambao tunao, mpaka leo tunategemea mataifa ya ulaya. Hata dhahabu, chuma, almasi, nickel na madini mengine yaliyopo chini ya ardhi yetu, bila ya wageni, hatuwezi kuyachimba, hata tukiyachimba, hatutakuwa na matumizi nayo.

Magufuli kama anataka nchi hii ipate maendeleo, akazanie sana uwekezaji. Lakini wawekezaji kwa maana ya wafanyabiashara, ni watu wa tahadhari kubwa (very sensitive). Mpaka sasa jamii kubwa ya wafanyabiashara hawana uhakika na serikali inataka kufanya nini, na ina mtazamo gani dhidi ya wafanyabiashara, biashara na uwekezaji. Huwezi kutamka kuwa, 'kuna watu walikuwa wanaishi kama malaika, nataka niwashushe waishi kama mashetani', halafu utegemee matajiri wawekeze. Je, utajiri nchi hii ni dhambi? Mimi nilitarajia Rais angesema kuwa waliokuwa wanaishi kama mashetani atawapandisha ili na wao waishi kama malaika! Niliwashangaa sana watanzania walioshangilia kauli ya Mheshimiwa Rais kuwa waliokuwa wanaishi kama malaika atawashusha ili waishi kama mashetani. Nikajiuliza, je, watanzania wanapenda na wanafurahia kuishi kama mashetani?

Mimi sipendi kuishi kama shetani, nataka niishi kama malaika. Rais aliomba ushauri, na ushauri wangu mkubwa ni kwamba serikali itusadie ili kwa jitihada za pamoja tuweze kuishi kama malaika. Lakini hili la kodi mrundikano na mnyororo litawafanya watanzania wote waishi kama mashetani, mtakaoishi kama malaika mtabakia ninyi pekee yenu mnaochukua kodi toka kwetu.
 
Point. Kuendesha nchi sio kama kulima kwa jembe la mkono ukatumia nguvu nyingi.
Tumetawaliwa na hofu ambayo imesababishwa na utawala huu.
Makosa waliofanya zaidi ya miaka 50 sasa wasitumie mbinu ambazo hazina tija kama kutafuta kurejesha imani kwa wananchi.

Walisema mtu mzima jiwe sasa ninaanza kuelewa kauli ya kuishiwa pumzi.
 
Umeongea point ila nakuonea huruma lumumba wakiuona Uzi huu jiandae na gunia la matusi na kashfa
 
Nahisi hata huko ndani ya CCM wanalaumiana wakati huu kuhusu uamuzi wa kumpa JPM usukani wa kuongoza nchi.Kuongozwa na rais ambaye ni clueless ktk mambo ya uchumi ni hatari kama bomu la wakati linalosubiri kulipuka muda wowote kule.Ukweli ni kwamba ataifanya CCM ichukiwe kuliko wakati wote na ataizamisha nchi ktk tope la umaskini.
 
"Simba na fisi waliopo Serengeti bila kuwa na akili ni laana maana kuna siku watakula wewe"..Hii nimeipenda sana mkuu, lakini kwa hali ilivyo sasa unaweza kuitwa mchochezi.
 
Namkumbuka kingunge alisemabkuwa hawa watu wameishiwa pumzi, alikuwa na maana kuwa hawewezi kuongoza.
 
Uchumi unatakiwa akili na kujua maeneo yapi ni sensitive...

Nchi haina export za kutosha......tuna import more than export...Zao la kahawa lilikuwa ndo export muhimu sana. Ilitakiwa serikali ifufue zao la kahawa na kutengeneza mazao mengine ya export kwanza.

Export products inaleta foreign currency......but Tanzania we have few and scarce export na hence hatuna forex za kutosha.


Ajabu sana...mfano umeshalipia shati,,,,,siku unaenda kuchukua.....unaambia shati imeongezewa VAT.....unapata wapi pesa za kuongezea kwa mfano? Budget conscious person wanajua hili....katika kipato chako....unapanga budget.....

Mzungu alishapanga budget ya Vacation trip Tangu 2014 au 2015 kutembelea Tanzania....Tourists save money to travel to certain destination and plan budget ahead. Kutalii sio anasa, ni utamaduni kwa wazungu...

Abruptly you come up with Additional VAT, without considering pre booked trips? You don't have any idea on Tourism Business?

Tourism runs Tanzania economy through Agriculture market and employment

TRA were not even prepared on Tourism on VAT.....

Miamala ya Pesa there is confusion between BOT and TRA...

Tourism infrastructure in Tanzania is poor compared to Dubai, Morocco, Mauritius, Egypt and yet you want rich tourists

After all rich tourists pays same park entry fee as middle class tourists...

Sote ni Watanzania, tunapenda kulipa kodi ili kuijenga nchi yetu...Mama Tanzania.....
 
In kama huko bandarini unaagiza gari mpaka unashindwa kuikomboa.
 
In kama huko bandarini unaagiza gari mpaka unashindwa kuikomboa.
 
18% VAT atalipa mwananchi anayetumia huduma kama mtumiaji wa mwisho. Hivi ndivyo ilivyo na sivinginevyo. Kwakifupi VAT inalipwa na mtumiaji wa mwisho wa bidhaa/huduma. Na hapa nakiri mwananchi wa kawaida amepata mzigo mzito kubeba. Exim bank walishatangaza wao watatoza 18% kila service utatumia.
 
Kwa ufupi sana iko hivi; kama 1m PAYE ni 200,000, kutoa salio lililobaki through ATM makato (kabla ya sheria mpya) ni 1,600. Kiasi kinachobaki (798,400) suppose chote umeenda kununulia mahitaji. Kwa 18% VAT maana yake makato ni 143,713. So, at very minimum, makato ya lazima kwa salary ya 1m ni sh. 345,313. Maana yake 35% ya mshahara ni kodi.
 
Back
Top Bottom