Mjomba Fujo
JF-Expert Member
- Oct 27, 2012
- 2,425
- 6,261
Written by Dr Francis Fredrick, MD
Imehaririwa na Dr Praxeda Swai, MD, MMED (Daktari bingwa wa afya ya akili)
Kwa kawaida huwa ni furaha kubwa isiyoelezeka kwa mwanamke kupata mtoto, na inasadikika hakuna furaha zaidi ya hiyo. Inapotokea mama wa mtoto kukosa furaha, kuwa mwenye huzuni na hasira, au hata kujiona mpweke, mwoga na mwenye kukosa upendo kwa mtoto hata kufikia kuwa na fikra za kumdhuru. Hizi zaweza kabisa kuwa dalili za tatizo la sonona baada ya kujifungua au kwa lugha ya kitaalamu postpartum depression.
Idadi kubwa ya wanawake (asilimia 30 mpaka 80) mara baada ya kujifungua hupatwa na hali za kuwa ha huzuni, wasiwasi, kukosa usingizi na kupungukiwa kwa hamu ya kula. Wanawake huweza pia kuwa na hali ya kubadilika badilika kwa hisia (mood swings). Kwa ujumla hali hii hujulikana kitaalamu kama maternal blues . Dalili hizi huwa kwa kiasi kidogo na mara nyingi huisha ndani ya muda mfupi.
"Endapo dalili zitaendelea kwa kipindi kinachozidi wiki mbili, basi hii yaweza kuwa dalili za sonona (postpartum depression)."
Tatizo la sonona hutokea baada ya mama kujifungua, mara nyingi ndani ya miezi 4 ya mwanzo, lakini linaweza pia kutokea wakati wowote katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kujifungua. Tafiti zinaonyesha kuwa katika wanawake kumi (10) wanaojifungua mmoja mpaka wawili (10-15%) hupatwa na tatizo la kukosa furaha kupindukia au kwa lugha ya kitaalamu sonona.
NINI DALILI ZA TATIZO HILI?
Dalili za tatizo hili hutokea wakati wowote kuanzia masaa 24 mpaka miezi kadhaa baada ya kujifungua. Dalili hizi ni pamoja na
• Kukosa furaha hata kwa vitu ulivyokuwa unavipenda, kuwa na huzuni inayokufanya ulie mara kwa mara na kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
• Kukosa nguvu, usingizi, hamu ya kula na kupungua uzito
• Kujiona mpweke, uliyetengwa na kuwa na mashaka na wasiwasi juu ya usalama wa mtoto
• Kujiona huna thamani na mwenye makosa, kutokuwa makini na kukosa uwezo wa kufanya maamuzi
• Kuwa na fikra hasi zikiwemo za kutaka kujiua au kumdhuru mtoto ikiwemo kumuua (hata hivyo ni mara chache sana kina mama wenye tatizo hili huwadhuru watoto wao au wao wenyewe)
Dalili hizi zinapokuwepo kwa muda mrefu bila ya matibabu zinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uwezo wa mama kumhudumia mtoto au watoto wake. Matokeo yake mama anaweza kufikiria kumuua/kuwaua watoto wake na hatimaye kujiua. Fikra hizi husababishwa na hofu na hisia za kutokuwa na uwezo wa wa kuwahudumia watoto na si kwa sababu ya chuki.
NINI KINAWEZA KUSABABISHA TATIZO HILI
Chanzo halisi cha tatizo hakijulikani, ila kuna vitu vinahusishwa na kutokea kwa tatizo hili. Vitu hivyo ni pamoja na:
o Mabadililiko ya homoni yanayotokea baada ya kujifungua. Kwa kawaida baada ya kujifungua kunatokea mabadiliko ya homoni hususani oestrogen, progesterone na cortisol.
o Historia ya ugonjwa wa sonona (depression) kabla ya ujauzito
o Migogoro ndani ya ndoa, kupoteza kazi, na kukosa msaada kutoka kwa ndugu na marafiki.
o Historia ya kuharibikiwa na mimba au kuzaa mtoto aliyefariki kipindi cha nyuma.
o Mabadiliko yanayotokea baada ya mama kujifungua yanaweza pia kuchangia kutokea kwa tatizo hili, Mabadiliko haya ni pamoja na:
Mambo yafuatayo yatakusaidia kukabiliana na tatizo hili:
WAKATI GANI NI MUAFAKA KUONANA NA DAKTARI/MTAALAMU
Ukiwa na dalili zifuatazo ni vizuri ukaomba msaada kwa ndugu aliye karibu na wewe au rafiki ili upate msaada wa awali na ikiwezekana upelekwe kuonana na mtaalam wa afya
Matibabu ya tatizo hili hutegemea vitu kadhaa ikiwemo ukubwa wa tatizo na hali inayoweza kuchangia kwa tatizo kutokea. Mtaalam wa afya ya akili au mwanasaikolojia anaweza kutoa aina mojawapo ya matibabu yafuatayo au kuyachanganya kwa pamoja;
Kwa kufanya yafuatayo unaweza kupunguza uwezekano wa kupata tatizo la sonona baada ya kujifungua

- Mabadiliko ya kimwili, yanayomfanya mama ajione tofauti, aliyepoteza mvuto wa kimwili
- Uchovu baada ya kujifungua
- Maumivu yanayotokea katika njia ya uzazi baada ya kujifungua
- Mawazo ya kukosa uhuru na kujiona aliyefungiwa nyumbani
- Hali ya kuelemewa na mzigo wa kuwa mama
- Msongo unaotokana na mabadiliko ya shughuli za nyumbani
Mambo yafuatayo yatakusaidia kukabiliana na tatizo hili:
- Kukaa karibu na ndugu au marafiki, waombe wakusaidie kumlea mtoto
- Angalia afya yako, pumzik akadri unavyoweza na ulale mtoto anapokuwa amelala
- Jitahidi ukae na watu waliopo nyumbani, usikae peke yako chumbani
- Tafuta muda ukae na mumeo peke yenu
- Jitahidi kuoga na kuvaa nguo kila siku
- Toka nje kwa matembezi, tembelea rafiki au fanya kitu unachokipenda. Tafuta mtu akusaidie kukaa na mtoto unapofanya haya, ikishindikana nenda na mtoto
- Usijichoshe kwa kazi za nyumbani, omba ndugu au marafiki wakusaidie
- Ongea na mama wengine wenye watoto na ujifunze kutokana na uzoefu wao.
WAKATI GANI NI MUAFAKA KUONANA NA DAKTARI/MTAALAMU
Ukiwa na dalili zifuatazo ni vizuri ukaomba msaada kwa ndugu aliye karibu na wewe au rafiki ili upate msaada wa awali na ikiwezekana upelekwe kuonana na mtaalam wa afya
- Ukiwa unajisikia huzuni sana kwa zaidi ya siku chache baada ya kujifungua
- Ukiona unashindwa kumudu kazi zako za kila siku, ikiwa ni pamoja na kumhudumia mtoto wako
- Kushindwa kulala kwa zaidi ya masaa mawili kwa siku
- Mawazo ya kujidhuru, kujiua au kumdhuru mtoto
Matibabu ya tatizo hili hutegemea vitu kadhaa ikiwemo ukubwa wa tatizo na hali inayoweza kuchangia kwa tatizo kutokea. Mtaalam wa afya ya akili au mwanasaikolojia anaweza kutoa aina mojawapo ya matibabu yafuatayo au kuyachanganya kwa pamoja;
- Ushauritiba (psychological help)
- Kupata msaada wa akina mama wengine wenye historia ya tatizo hilo (group therapy)
- Ushauri wa ndoa, iwapo kuna migogoro ya kifamilia
- Matibabu ya dawa kadri mtaalam atakavyoona inafaa.
- Mama kushindwa kumlea mtoto wake ipasavyo hivyo kupelekea kushindwa kukua vizuri kiakili na kimwili
- Kumuumiza au kumuua mtoto
- Mama kujiua
- Kuvurugika kwa mahusiano ndani ya ndoa au familia
- Mama kushindwa kumudu majukumu yake ya kila siku katika familia au ya kikazi
- Hali ya kuchanganyikiwa
Kwa kufanya yafuatayo unaweza kupunguza uwezekano wa kupata tatizo la sonona baada ya kujifungua
- Kuongea na mtu wako wa karibu ili kupata utatuzi wa hali yoyote inayokuletea msongo wa Mawazo (stress) wakati wa ujauzito au mara baada ya kujifungua
- Kupata muda wa kutosha kupumzika baada ya kujifungua
- Kuomba msaada pale unapoona unazidiwa na majukumu ya kumlea mtoto au ya kifamilia
- Familia na hasa mwenza awe karibu sana na mama aliyejifungua hasa katika kipindi cha mwanzoni kwa ajili ya kumpa msaada wowote atakaohitaji ili aweze kupumzika
- Mama asiwe na mategemeo yasiyo halisia kuhusiana na malezi ya mtoto wake mtoto mchanga
- Kuyakubali mabadiliko ya kimaumbile yanayotokea kipindi cha ujauzito na hata baada ya kujifungua
- Kujiandaa na kuyakubali majukumu ya kuwa mama na kuomba msaada pale unapoona umeelemewa.