mgosi agosigwa
Member
- Dec 4, 2013
- 24
- 4
Siku hizi sijui nini kimeikumba jamii yetu au labda kinanikuta peke angu tu!! Unakuta mtu anakuja kukulilia umkopeshe hela na stori kibao za matatizo anayoyaface akiahidi atakulipa baada ya muda flan..aisee ukimpa ujue kama umetoa msaada maana kulipa inakua ishu sana, hata sometimes mtu anajifanya hakumbuki kama alishakopa.ukimuuliza utaskia" mambo hayajaa fresh ntakupa tu mzigo wako!" Sasa unabaki kujiuliza, ina maana huyu jamaa alikuwa anasubiria mpaka nimuulize kuhusu mzigo wangu au? Sasa ndo usubiri kama atarudisha hiyo pesa, sahau!!Hii tabia inakera sana