Kukatika hovyo kwa umeme na ujambazi Kigamboni

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Wiki hii maeneo kadhaa ya mji wa Kigamboni watu wamekumbwa na ujambazi.

Jambo la kushangaza ni kwa shirika la Tanesco kuwa kikwazo kikubwa kwa wakazi maana kwa majuma kadhaa usiku wa manane umeme unakatika hata mara 4 na kuwaka yaani utadhani kuna mtoto anachezea switch.

Katika giza totoro la vichochoro vya Kibada, Mikwambe na ToaNgoma tatizo la wizi limekuwa likibebwa na giza hili la makusudi.

Wakazi tunapata shida kujua Tanesco kulikoni mtuzimie umeme usiku wa manane karibu kila siku?

Mbona mchana mnatoa tahadhali kwa tatizo la umeme, lkn hili la usiku mpo kimya, limekuwa sugu na pia lina hatarisha usalama wa raia, mali zao na askari wanaokuja kutoa msaada!

Tunawaomba Tanesco watusaidie, pia mbunge wetu tusaidie!

Lakini tuwaombe wakazi wa kigamboni, kama tatizo hili likiendelea, tupange siku ya kufanya mkutano na wawakilishi wetu wawaone mkurugenzi mkuu wa Tanesco na waziri mwenye dhamana,. hatuwezi kuweka rehani roho zetu kwa kiasi hiki...!
 
Hivi huku Kigamboni tunaadhibiwa au, toka huu mwaka uanze umeme unakatika mara 20 kwa siku! Tatizo nini?
 
Siyo kigamboni peke yenu huku mitaa yetu ya mbagala chamazi ndio kumezidi kwa mgao wa umeme
 
kuna mgawo wa chini chini ila wanaogopa kusema wasije wakakutana na ghadhabu za Mkubwa asiyependa kuambiwa matatizo!

Nunua koroboi tu mkuu kama wewe si mpiga dili
 
Back
Top Bottom