Kujitibu Mwenyewe (Self Medication)

osc michael

Member
Sep 10, 2017
49
75
Kujitibu mwenyewe ni hali ya kuamua kutumia dawa kulingana na ugonjwa au dalili za ugonjwa ambazo mtu anazisikia au anahisi na kuzifahamu yeye mwenyewe pasipo kupata maelekezo ya mtaalam wa Afya.

UKUBWA WA TATIZO
Takwimu za Shirika la afya Duniani (WHO) za mwaka 2015 zimeonesha 80% ya watu (ikiwemo Tz) wanajitibu wenyewe.

SABABU
  • Gharama za matibabu
  • Kutumia muda mrefu kupata matibabu kutokana na wingi wa wagonjwa katika kituo cha kutolea huduma za afya
  • Mgonjwa kutumia dawa zilizobakizwa ama kuachwa na mgonjwa mwingine.
  • uelewa mdogo juu ya madhara yanayoweza kusababishwa na mgonjwa kujitibu mwenyewe
  • Vituo vya kutolea huduma za afya kuwa mbali na jamii kwa baadhi ya maeneo
  • Kutokuwa na Bima na Afya
ATHARI
  • Mgonjwa kutokupona
  • Usugu wa dawa aina ya vijiuasumu (antibiotic)
  • Kusababisha ulemavu na hata kifo
  • Kuongezeka kwa gharama za matibabu kwa Taifa na jamii kwa ujumla
NI MUHIMU
Usijitibu wala kutumia dawa bila ushauri wa daktari.
 
Back
Top Bottom