Na Dokta Paulo Matemu.
1. hicho ni kitendo binadamu kutoa hewa chafu inayotokana na bacteria rafiki waishio kwenye utumbo.
2. Ile hewa harufu yake inategemeana na mlo. Vyakula vyenye protein sana husababisha harufu kali. Au mtu akila na kuzidisha hivyo kuvimbiwa. Huweza kusababisha hewa hiyo ikapitia mdomoni pia.
3. Ile hewa huwa ina Ammonia, Sulphide, carbon dioxide na methane
4. Wapo watu wanaweza kujizuia wasijambe. Nb. Ni mbaya kiafya. Tafuta sehemu hakuna mtu jamba. Ondoa hewa chafu mwili. Hivi kwa nini wahenga walifanya kitendo cha kujamba kionekane ni cha aibu?
5. MADHARA ya KUJIZUIA KUJAMBA ni
5. a. Utumbo unatanuka na kutuna... unatengeza vibox ambavyo ndani yake kunaingia uchafu ( mabaki ya chakula yaani choo) na bacteria hewa ikija kutoka penyewe panajibana na kusababisha ugonjwa uitwa diverticulatis....
5. b. Unaweza kuvimbiwa
5. c. Utumbo unaweza kujaa gesi na ghafla ukajizungusha kusababisha volvulus hatimaye utumbo kuziba. Matibabu ni operesheni. Hii inawatesa sana wanaume.
5. d. Huweza kusababisha kiungulia
6. Usipojamba kwa siku 3 mfululizo ujue kuna tatizo la kiafya ktk mfumo wa chakula. Unaweza usijue umejamba lakini ukiwa usingizini au bila kujua hewa inatoka