Kuitwa kwenye usahili Arusha Technical College

MAUBIG

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,035
854
Chuo Cha Ufundi Arusha kinatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwaajiri waombaji watakaofaulu usaili kama ilivyoonyeshwa hapa chini. Wasailiwa lazima wazingatie yafuatayo:

1. Kuja na vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji
2. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
3. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
4. Kila msailiwa azingatie tarehe aliyopangiwa.
5. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate). 6. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
7. Wale ambao walisoma nje ya Nchi wahakikishe kuwa vyeti vyao vinapata ithibati ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
8. Wale ambao wana Ajira rasmi waje na barua za ruhusa kutoka kwa waajiri wao.
9. Tangazo hili linapatikana pia katika tovuti ya Chuo: - www.atc.ac.tz


Chuo Cha Ufundi Arusha kinawatangazia wafuatao kuwa wanahitajika kwenye usaili kwa nafasi walizoomba ambazo zilitangazwa tarehe 23 Februari, 2016. Usaili utafanyika Chuo cha Ufundi Arusha tarehe 26 na 27 Mei, 2016 saa mbili kamili (2:00) Asubuhi. Aidha tarehe ya usaili imeainishwa kwa kila nafasi, hivyo wasailiwa wote mnatakiwa kuzingatia tarehe husika.


PAKUA FILE HILO HAPO CHINI KWA KUWEZA KUONA KAMA UMEITWA KWENYE INTERVIEW
 

Attachments

  • CALLFOR INTERVIEW 2016.pdf
    1.3 MB · Views: 346
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom