Kuitoa CCM madarakani,tunahitaji viongozi aina ya Godbless Lema kuongoza vyama vya upinzani

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,682
149,883
Niliwahi sema siku za nyuma ila leo narudia hasa baada ya kauli inayodaiwa kutolewa na Magu kuwa wapinzani wasahau kutawala nchi hii.

Niwambie tu ukweli wenzangu mnaotamani mabadikiko,viongozi aina ya Mbowe,Mbatia, Lowassa na wengineo kama kina Zitto n.k, hawawezi tena kuendesha harakati za kudai haki kwa mambo yanayokwamisha demokrasia ya kweli hapa nchini kama vile kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi,Mgombea binafsi,n.k.Tumekosa viongozi "aggressive" wa vyama vya upinzani.

Mbowe,Mbatia,Zitto na viongozi wengine wa vyama upinzani wanaweza tu kudai haki hii kupitia meza ya majadiliano.Lakini je,CCM wako tayari kurekebisha kasoro hizi kupitia meza ya majadiliano?Tumejifunza nini kuhusiana na mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Zanzibar? Bado tu tunahitaji ushahidi zaidi ya huu?

Tunahitaji watu wenye fikra, mawazo, mitazamo na guts za watu kama kina Godbless Lema kuongoza vyama vya upinzani na pia kuongoza harakati za kweli za kupiganja demokrasia katika nchi hii.

Hizi lugha za kiburi ni matokeo ya kujiamini kuwa watanzania wamelala na hakuna viongozi wa upinzani wenye ubavu wa kuongoza harakati za kweli kupigania demokrasia ya kweli.
 
Bila ya watu kama kina Lema wenye misimamo na wasio rudi nyuma hatuwezi kamwe kuheshimiana
Nilitaka kupuuzia ulipoambiwa kuwa siku hizi unatumia common sense, ila kwa post hii naanza kuamini - kweli unatumia common sense.

Lema huyu anayebadirika kama kinyonga , kwa miaka minane alituhamasisha tumpige mawe Lowasa endapo tutakutana naye, leo anatumbaia tuungane kuzungusha mikono? Hivi Lema ana msimamo gani hasa?
 
Niliwahi sema siku za nyuma ila leo narudia hasa baada ya kauli inayodaiwa kutolewa na Magu kuwa wapinzani wasahau kutawala nchi hii.

Niwambie tu ukweli wenzangu mnaotamani mabadikiko,viongozi aina ya Mbowe,Mbatia, Lowassa na wengineo kama kina Zitto n.k, hawawezi tena kuendesha harakati za kudai haki kwa mambo yanayokwamisha demokrasia ya kweli hapa nchini kama vile kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi,Mgombea binafsi,n.k.Tumekosa viongozi "aggressive" wa vyama vya upinzani.

Mbowe,Mbatia,Zitto na viongozi wengine wa vyama upinzani wanaweza tu kudai haki hii kupitia meza ya majadiliano.Lakini je,CCM wako tayari kurekebisha kasoro hizi kupitia meza ya majadiliano?Tumejifunza nini kuhusiana na mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Zanzibar? Bado tu tunahitaji ushahidi zaidi ya huu?

Tunahitaji watu wenye fikra, mawazo, mitazamo na guts za watu kama kina Godbless Lema kuongoza vyama vya upinzani na pia kuongoza harakati za kweli za kupiganja demokrasia katika nchi hii.

Hizi lugha za kiburi ni matokeo ya kujiamini kuwa watanzania wamelala na hakuna viongozi wa upinzani wenye ubavu wa kuongoza harakati za kweli kupigania demokrasia ya kweli.
Well said Salary Slip,
ila kuna baadhi ya watu wenye mioyo migumu hawawezi kukubaliana na hili.
 
Hivi kweli kati ya Lema na Mbowe ni yupi jembe huko CHADEMA? Mtoa mada unataka kuitwa msaliti sio?
 
Well said mkuu siasa za mezani ccm watatubuluza sana maana wameshatuona wa tz wote vilaza! Lema. Sugu,Lissu na mdee they can wapewe chama
 
Kwa mawazo yangu Mbowe anaweza kurithiwa na Profesa Baregu pamoja na Profesa Safari, kama viwango vya uongozi ni busara, elimu , hekima na uzoefu wa mambo ya siasa. Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa kiongozi wa chama na mwanaharakati wa chama. Sifa kubwa ya mtu kuweza kuongoza chama cha siasa ni kuwa na kitu ambacho wazungu wanakiita CHARISMA, yaani ule mvuto mkubwa wa kuweza kuwafanya watu wakakuamini.

Mbowe ana Charisma kubwa sana, ndio maana alipoanzisha mtindo wa kuvaa gwanda, maelfu ya wanachadema wakamuiga, wapo viongozi wengi wa CHADEMA ambao wanajaribu hata kuiga mtindo wake wa kuongea. Mwalimu Nyerere alikuwa na charisma kubwa sana. Katika upinzani Zitto Kabwe ndio mwenye kufanana na Mbowe katika suala la Charisma.

CHADEMA imejaa wanaharakati wa chama, wanasiasa wanaoishi kwa kutegemea milipuko ya matukio ya kisiasa na kijamii, hawa hawana uwezo wa kumrithi Mbowe, baadhi yao ni Godbless Lema, Tundu Lissu, John Mnyika, Halima Mdee, Mchungaji Msigwa, na Mbilinyi "sugu". Freeman Mbowe kama binadamu anao udhaifu wake mwingi tu, lakini kumlinganisha na hao wanaharakati niliowataja ni kumkosea adabu.
 
Hivi kweli kati ya Lema na Mbowe ni yupi jembe huko CHADEMA? Mtoa mada unataka kuitwa msaliti sio?
Viongozi wakweli wa upinzani bado hawajapatikana. Waliopo ni wenye uchu wa madaraka (kutumikiwa) na siyo kuitumikia nchi hii. Vyama vya upinzani vinaanzishwa kwa lengo la kuingia Ikulu (kupata ulaji) na siyo kuleta maendeleo kama ilivyokuwa TANU kuwakomboa Watanzania kutoka ukoloni.

Tunachokishuhudia kwa viongozi wa sasa wa vyama vya siasa ni hoja za chuki (kugonganisha wananchi na viongozi wa serikali iliyoko madarakani).

Mfano wabunge wa Upinzani walikuwa vinara wa miongozo bunge lililofungwa jana. Baadhi ya miongozo hiyo haina tija kwa taifa zaidi ya mbunge kujitafutia umaarufu.

Hii hapa baadhi ya miongozo ya masuala ambayo kwa uhakika Serikali ilikuwa au ni budi iyashughulikie pasipo haja ya kuzungumzwa bungeni:
1) Zitto (akiungwa mkono na Lissu) alihoji TBC kutorusha moja kwa moja matangazo ya shughuli za bunge - suala ambalo mbunge angeweza kulifikisha kwa TBC yenyewe. Kibaya zaidi ni pale alipohusisha matumizi mabaya ya kodi ya wananchi inayoendesha TBC akisahau pia kwamba wao hususia mijadala wakati huohuo wanalipwa posho ambazo ni kodi za wananchi.
2) Kubenea yeye aliomba mwongozo kupinga kuwa TFF ni chombo cha muungano. Pia hili swala limejadiliwa sana na vyombo husika na limepitwa na wakati. Linaweza kujadiliwa kwa undani kwenye mjadala wa Katiba ambayo bado haijaridhiwa.

UPINZANI UCHAMBUE MASUALA YA KITAIFA UCHUNGUZE UAMUE UCHUKUE HATUA
 
Niliwahi sema siku za nyuma ila leo narudia hasa baada ya kauli inayodaiwa kutolewa na Magu kuwa wapinzani wasahau kutawala nchi hii.

Niwambie tu ukweli wenzangu mnaotamani mabadikiko,viongozi aina ya Mbowe,Mbatia, Lowassa na wengineo kama kina Zitto n.k, hawawezi tena kuendesha harakati za kudai haki kwa mambo yanayokwamisha demokrasia ya kweli hapa nchini kama vile kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi,Mgombea binafsi,n.k.Tumekosa viongozi "aggressive" wa vyama vya upinzani.

Mbowe,Mbatia,Zitto na viongozi wengine wa vyama upinzani wanaweza tu kudai haki hii kupitia meza ya majadiliano.Lakini je,CCM wako tayari kurekebisha kasoro hizi kupitia meza ya majadiliano?Tumejifunza nini kuhusiana na mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Zanzibar? Bado tu tunahitaji ushahidi zaidi ya huu?

Tunahitaji watu wenye fikra, mawazo, mitazamo na guts za watu kama kina Godbless Lema kuongoza vyama vya upinzani na pia kuongoza harakati za kweli za kupiganja demokrasia katika nchi hii.

Hizi lugha za kiburi ni matokeo ya kujiamini kuwa watanzania wamelala na hakuna viongozi wa upinzani wenye ubavu wa kuongoza harakati za kweli kupigania demokrasia ya kweli.
kwanini msianzishe chama chenu then mfanye haya mnayoshauri wengine?
 
Mbowe hakuna mbabe wake nyie watu tuache kufikr kidg ndg zangu mbowe mtazamo.wangu yuko.imara lkn pia ni bnadam kumbukeni
 
Back
Top Bottom