Kuiombea amani nchi yetu Tanzania miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,611
Amani ni kitu cha thamani kubwa sana. Ukitaka kuujua ukweli kwamba hali ya kutokuwepo kwa amani, ni kikwazo cha maendeleo na ustawi wa jamii nzima, tazama jinsi ambavyo wakimbizi wengi barani Afrika wanavyowasili kwenye nchi wanazokimbilia wakiwa wameweka kila walichonacho kwenye viroba vilivyochakaa. Ukiwatazama wakimbizi hao haswa jinsi ambavyo kinamama wanapata wakati mgumu kuwabeba watoto wadogo migongoni na wengine mikononi huku wakihakikisha kunakuwepo na usalama wa familia, ndipo utagundua uzito na thamani halisi ya amani.

Miaka ya karibuni imezuka tabia ya taasisi za dini kuandaa ibada maalum za kuombea amani ya nchi, na ibada hizi mara nyingi huanza kuzungumziwa ndani ya miezi michache kuelekea uchaguzi mkuu. Viongozi wa dini na wanajamii wenye nia njema na nchi ya Tanzania, huwa mstari wa mbele katika kuratibu shughuli zote kuelekea siku maalum ya kuomba amani. Watu huacha shughuli zao ili waweze kuwa sehemu ya jumuiko maalum litakalo kesha usiku kucha likiiombea Tanzania ipite katika kipindi cha uchaguzi kwa amani.

Baada ya uchaguzi kufanyika na washindi kujulikana, kila mtu huonekana kuchukua hamsini zake. Uonevu kwenye jamii hurudia pale pale, wapigaji kwenye mashirika hurudia pale pale. Ile amani tunayomuomba Mungu aweze kutuongoza ili iendelee kuwepo, thamani yake ni ile miezi michache baada ya uchaguzi na tukishamaliza uchaguzi kila mtu na lwake au inao umuhimu wa kuendelea kuwepo maishani mwetu?. Ikiwa tunaweza kujipanga na kuandaa mkesha wa kuombea amani ya Tanzania, hatuwezi kweli tukiwa katika spirit hiyo hiyo kuepuka kufanya yale yote ambayo hutupatia uoga wakati wa ile miezi michache kuelekea uchaguzi mkuu?.

Kuna maisha baada ya uchaguzi mkuu ni kweli kabisa, lakini pia kuna utendaji wa haki unaopaswa kuwepo baada ya uchaguzi mkuu ili tunapokaribia nyakati za uchaguzi tusiwe na hofu za ziada kuhusiana na hatima ya shughuli zetu za kimaisha. Waungwana haya ni mawazo yangu.
 
Huenda wakati huo miezi michache kabla ya uchaguzi anakuwepo mungu maalumu kwa ajili ya amani ya uchaguzi tu. Baada ya uchaguzi mungu huyo nae anaondoka zake hadi kipindi kingine tena cha uchaguzi. Vinginevyo huo utaratibu ungeendelea baada ya uchaguzi.
Mungu wa kweli alitupa amani bure wala hatukuiomba, ni bure. Tunavuruga na kuharibu kile alichotupa Mungu wenyewe halafu tunaangaika tena kumwomba Mungu aturejeshee. Hii sawa na baba aliyempa mwanae zawadi nzuri na huyo mtoto kwa vile hajui thamani ya hiyo zawadi akaamua kuitupa. Baadaye anapokuja kugundua kuwa alitupa kitu cha thamani anarudi kwa baba yake kuomba tena.
Viongozi wanavuruga amani halafu wanapanua midomo yao eti waombewe......!!!
 
Back
Top Bottom